Breaking News

Jan 3, 2022

CCM MOROGORO WARIDHISHWA NA UJENZI WA MADARASA YA COVID 19

 


CCM MKOA WA MOROGORO WARIDHISHWA NA UJENZI WA MADARASA YA COVID  19

Na Thadei Hafigwa

UJENZI wa vyumba vya madarasa 707 kwa shule za sekondari zilizopo katika mkoa wa Morogoro uliotokana na mpango maalum na fedha za covid 19 umekamilika na kugharimu zaidi ya  shilingi 14, ambapo wananchi na wadau wa elimu wametakiwa kumuunga mkono serikali ya awamu ya sita katika jitihada zake za kupunguza kero za wananchi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro,Dorothy Mwamsiku amesema hayo  wakati akiongea na waandishi wa habari kwamba kamati ya siasa mkoa wa Morogoro wamekuwa katika ziara ukaguzi wa ujenzi wa madarasa ya sekondari mkoa mzima katika wilaya 7 zilizopo mkoani hapa ambako kamati ya siasa kuridhishwa na fedha zilizotumika kwamba kasi ya ujenzi uliendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

“Kamati ya siasa mkoa umefanya ziara katika wilaya zote hapa Morogoro kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mpango wa covid 19 wa  maendeleo katika sekta ya elimu kwamba tumeridhishwa na vyumba 707 vilivyojengwa baada ya kupokea fedha kutoka serikali kuu.”Alisema Mwamsiku.

Mwamsiku amesema kuwa katika mkoa wa Morogoro walipokea fedha kutoka serikali kuu shilingi bil.20,250,000,000 kwa ajili ya kuboresha huduma ya elimu na afya kati ya fedha hizo bil.14,140,000,000 zilitumikwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa wote wa Morogoro ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM ya kuwahudumia wananchi.

Aidha,Mwenyekiti huyo wa CCM mkoani hapa alimpongeza  Rais Samia Suluhu kwa kuonesha mfano wa utawala bora kwani toka alipoingia madarakani amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa uwazi na kuwafanya wananchi kutambua mipango mbalimbali inayofanywa na serikali .

Alisema msimamo chama cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro ni kumuunga mkono Rais Samia kutokana na moyo wake wa kizalendo aliokuwa nayo na kwamba watasimama kidete usiku na mchana kupingana na watu wachache wasiitakia mema taifa na kumrudisha nyuma jitihada za kuleta maendeleo. 

Kuhusu   chanjo ya covid 19,Mwamsiku amesema toka chanjo hiyo ilipozinduliwa mkoani hapa Agosti 3,mwaka jana mwamko kwa wananchi kujitokeza kupata chanjo bado upo chini kwa kile alichokieleza licha ya kuwa lengo ilikuwa ni kuchanja watu 1,679,556 lakini hadi sasa ni watu 104,221 pekee kati yao wanawake ni 49,630 huku wanaume wakiwa 54,609 waliojitokeza kwenye vituo vya afya na  kupata chanjo hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuwahimisha wananchi mkoani hapa kujitokeza kwenye vituo vya afya na hospitali ili waweze kupata chanjo dhidi ya covid 19 kwa kuwa ugonjwa huo upo na unaua,hivyo kila mwananchi anapaswa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kutumia barokoa,vitakasa mikono na kupata chanjo ili waweze kuwa salama na kulifanya taifa liwe imara na watu wake lenye afya bora.

No comments:

Post a Comment