Na Thadei Hafigwa
MASHIRIKA
yasiyo ya Kiserikali hapa
nchini yametakiwa kuzingatia sheria kwa kuwasilisha taarifa kwa msajili kwa
wakati ili kuepuka mikwamo ya uendeshaji wa shughuli za kuibudumia jamii huku
wakitakiwa kuondokana na hofu wakati serikali ikiwa katika kuboresha mifumo
itakayorahisisha utoaji wa vibali katika ngazi ya serikali za mitaa.
Mkurugenzi, ofisi ya msajili wa NGO,Wizara ya
Afya,Mussa Sanganya alitoa rai hiyo Mjini Morogoro wakati wa Mkutano maalum
uliyokutanishwa mashirika yasiyo ya Kiserikali yaliopo Mkoa wa Morogoro ili
kuboresha mahusiano kati ya serikali na mashirika hayo,Mkutano ulioratibiwa na
Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Serikali Mkoa wa Morogoro(UNGO)
Sanganya alisema ya kuwa licha ya kuwepo na changamoto
mbalimbali za kiutendaji kwa siku za nyuma lakini kwa sasa serikali imeboresha
mifumo yake kwa kuwarahisishia wananchi wanaotaka kusajili NGO kwa kuweka
mifumo yote kwa njia ya mtandao.
“serikali ilitambua changamoto mnazozipata wakati wa
zoezi la usajili wa NGO,wananchi walikuwa wakipata usumbufu wa kuja wizarani
kushughulikia usajili,inapobainika nyaraka zao kuwa na dosari wanalazimika
kurudi walipotoka ili kuzirekebisha,adha hiyo kwa sasa haipo tena kila kitu
kipo kwenye mtandao na usajili unafanyika huko huko walipo.”Alisema Sanyang
Alisema serikali
inatambua mchango wa asasi za kiraia kwamba serikali inatimiza wajibu wake na
kuyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kutimiza wajibu wao ili kuihudumia
jamii hasa zinazoishi pembezoni.
MWENYEKITI WA UMOJA WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI MKOA WA MOROGORO(UNGO),DEOGRASIA IGNAS AKITOA TAARIFA YA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MINNE KWA WAJUMBE WA WALIOSHIRIKI MKUTANO HUO(HAPO PICHANI)
Awali,Mwenyekiti wa umoja wa Mashirika yasiyo ya
Kiserikali Mkoa wa Morogoro (UNGO),Deograsia Ignas alitoa taarifa ya mkakati wa
miaka minne ikiwemo kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuanzisha program za
kuhamasisha amani na utengamano wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo
wanaofanyakazi mkoani hapa.
Deograsia,amesema kuwa Mtandao wa Mashirika yasiyo ya
Kiserikali itahkikisha ya kuwa inawahudumia jamii kwa kuhakikisha mitandao ya
NGO iliopo Wilayani inaimarika kimifumo na kutoa mchango mkubwa wa kuhudumia
wanachama wake ili jamii iweze kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa UNGO,Dk.Saidi Simoni
alisema kuwa Mtandao huo imesajili kisheria mwaka 2000 kwa namba ya usajili
SO.NO.10101 ambapo ilipita katika awamu
tofauti za utekelezaji wa shughuli za kuihumia jamii kwa kuibua miradi
mbalimbali katika ufuatiliaji wa rasilimali za umma na usimamizi wa fedha.
Katika Mkutano huo uliojumuisha wadau mbalimbali wa
mashirika yasiyo ya kiserikali yaliopo hapa nchini na mashirika yakimataifa
walielezea changamoto mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira na changamoto
wanazokabiliana nazo ikiwemo jamii yenye ulemavu wa afya za akili kukokosa
fursa za kurahisishiwa katika uundwaji wa vikundi vyao.
BAADHI YA WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKIFUATILIA KWA KARIBU HOJA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA NA VIONGOZI
Venance Mlali Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake Mafiga
lililopo Manispaa ya Morogoro alisema kuwa jamii yenye changamoto za afya ya
akili wanajikuta kwenye wakati mgumu katika kukabiliana na matakwa ya
kiserikali wakati wa kuundwaji wa vikundi vyao hivyo alipendekeza kuwa ni muda
muafaka kwa serikali kuangalia namna bora ya kuwarahisishia kundi hilo ambalo
limeonekana kusahaliwa.
WASHIRIKI WA MKUTANO MAALUM WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI MKOA WA MOROGORO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKURUGENZI IDARA YA USAJILI WA NGO,WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO,MUSSA SANGANYA
Nzuri!
ReplyDelete