Breaking News

Apr 6, 2025

WALIMU MANISPAA MOROGORO WATAKIWA KUWA WAMOJA

 


Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Musa Kilakala

WALIMU MANISPAA MOROGORO WATAKIWA KUWA WAMOJA

Na Thadei Hafigwa

WAJUMBE wa mkutano mkuu 113 wa Chama Cha walimu manispaa ya Morogoro wametakiwa kuwa wamoja na kushikamana licha ya kutofautiana kwa kimtazamo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mororogo,Muda Kilakala wakati wa kufungua mkutano mkuu maalum ulioendavsambamba na uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho

Kilakala aliwaasa wajumbe kutambua kuwa Kuna maisha baada ya uchaguzi,hivyo kuwepo kwa uchaguzi kusiwe chanzo  Cha kuwagawa walimu kwa kuwa walimu wana dhamana kubwa kwa jamii katika kuwafundisha wanafunzi kitaaluma.

"baada ya mkutano huu,mkishapata viongozi wenu changamoto mlizonazo tutajadiliana kwa pamoja kwa kuwajumuisha wakuu wa Idara kutoka halmashauri pamoja na Mkurugenzi"alisema

Mwenyekiti wa CWT Manispaa ya Morogoro aliyemaliza muda wake Gaspar Jaka akitoa neno wakati wa mkutano huo.

Awali,Gaspar Jaka Mwenyekiti wa Chama hicho manispaa yaorogoro aliyemaliza muda wake alisema kuwa Chama Cha walimu kitaendelea kushirikiana na serikali kwa kufanyakazi kwa bidii bila ya kuchoka.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Morogoro,Jumanne Nyakirang'ani akitoa nasaha zake katika mkutano huo.


Katika mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa wafanyakazi sehemu za kazi ambao mchakato wake ulizingatia demokrasia,kwa kuwawajumbe ni ngazi ya kwanza ya utetezi ambao ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wilaya na wafanyakazi wenzao.

Aidha,wajumbe walipitia taarifa za utendaji wa kazi ya miaka mitano pamoja na mapato na matumizi,sanjari na kuwachagua viongozi wa chama chao katika nafasi ya Mwenyekiti,mwekahazi na wajumbe wa kamati tendaji.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Morogoro,Jumanne Nyakirang’ani ambaye alielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu waliopo katika halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na manispaa ya Morogoro.

Nyakirang’ani alionesha kuridhishwa kwake na uamuzi wa serikali kwa kufungua madaraja ya walimu sambamba na kubadilisha muundo wa utumishi.

Aidha,miongoni mwa watendaji wa kazi wa serikali ni pamoja na Maafisa utumishi na ofisi ya TSC Wilaya ambao walishughulikia suala la marejesho kwa kuwa katika wilaya hiyo changamoto ya kusahaulika walimu katika upandaji vyeo ni ndogo ukilinganisha na wilaya nyingine.


”chama chetu kimepiga hatua kubwa katika jitihada za kutetea haki na masilahi ya walimu ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa wanachama na kuwajengea uwezo wa kudahi haki zao.”alisema

Katika Mkutano huo,walimu wa wilaya ya Morogoro walianisha mafanikio ambayo wameshughulikiwa na serikali ya awamu ya sita kwa kupandishwa madaraja walimu.

Serikali imetoa ruzuku ya fedha ya likizo mara mbili kila mwaka hivyo walimu wanakwenda likizo japo fedha zinazotolewa katika wilaya hiyo hazichosherezi idadi ya walimu waliopo.

Hata hivyo,changamoto zinazowakabili walimu ni pamoja na madeni ya uhamisho yanayotokana na malimbikizo ya mishahara tangu mwaka 2014 hadi sasa walimu 621 wanadai bila ya mafanikio na madai yao kutopandishwa katika mfumo japo wamejaza fomu za maombi ya malipo zaidi ya mara moja.

Katibu wa CWT Manispaa ya Morogoro,George Lukoa akielezea umuhimu wa mkutano huo uliojumuisha wajumbe 113

George Lukoa katibu wa CWT manispaa ya Morogoro alionesha kuridhishwa na maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Musa Kilakala katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili walimu.

Lukoa alisema kuwa ofisi yake itaendelea kuwahudumia walimu na kuwahimiza wanatekeleza wajibu wao wakati serikali ikiendelea kuzipatia majawabu.

No comments:

Post a Comment