KULA PILIPILI KALI HAKUPONYI,KUZUIA COVID-19-WHO
Na Deogratius Chechele
WAKAZI wa Gairo Mkoa
wa Morogoro wamekuwa wakitumia pilipili nyingi wakati wa covid kwa dhana kwamba
ulaji wa pilipili kwa wingi huenda kuna saidia kupambana na covid 19.
Mwandishi wa habari hizi amepita katika soko na magulio mbalimbali Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro na kubaini ya kuwa wananchi wamekuwa wakifanya biashara kubwa ya pilipili huku kukiwa na dhana kuwa pikipili zinasaidia kupambana na covid 19.
“Pilipili zimeonekana kuwa na soko kubwa kutokana kupendwa na watu kwa kile kilichoelezwa kuwa radha yake huenda ikasadia watumiaji kukabiliana na makali ya covid 19” alisema mfanyabiashara mmoja wa pilipili aliyejitambulisha kwa jina Goloko Juma.
Hata hivyo radha ya
pilipili ambayo ni yenye muasho, lakini haziwezi kuzuia au kuponya COVID-19 kwa
mujibu wa shirika la afya duniani.
Shirika la afya duniani,ambapo hivi karibuni
wamebainisha ya kuwa njia bora ya kujilinda dhidi ya COVID-19 ni kukaa mbali na
wengine na kusafisha mikono yako mara kwa mara na kabisa.

No comments:
Post a Comment