Breaking News

Feb 2, 2021

KULA KITUNGU SAUMU KUPUNGUZA MAKALI,HAKUZUA, KUTIBU COVID-19?

 


KULA KITUNGU SAUMU KUPUNGUZA MAKALI,HAKUZUA, KUTIBU COVID-19?

Omar Hussein

WANANCHI wa Mjini Morogoro hivi karibuni walijikuta wakitumia vitunguu saumu kwa dhana kwamba ni moja ya chakula cha kukabiliana na ugonjwa wa covid 19.

Mmoja wa wakazi wa Mjini Morogoro Maria Mkude alisema kuwa anaishukuru sana serikali kwamba imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ya kuwa ugonjwa wa covid hauleti madhara makubwa kama ilivyo nchini nyngine duniani ambapo hadi sasa wanakabiliwa na ugonjwa wa covid huku biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi zikirora.

Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani zinaeleza kuwa Kitungu saumu kwamba licha ni chakula chenye afya kinachoweza kuuwa baadhi ya viini, lakini hakuna ushahidi wowote kwamba kinawalinda watu dhidi ya COVID-19. Njia bora ya kujilinda dhidi ya COVID-19 ni kukaa mbali na wengine na kusafisha mikono yako mara kwa mara na ipasavyo.

Hata hivyo, soko la tangawizi limekuwa kubwa katika masoko ya mjipya,mawezi na soko kuu la Morogoro,kutokana na dhana kwamba ni miongoni mwa vyakula vinavyopatikana kwa urahisi na vina saidia kupunguza makali ya covid 19.

WATALAMU WA KILIMO KILIMO BORA CHA KITUNGUU SAUMU NA MACHAPISHO MBALIMBALI

Kitunguu saumu kwa lugha ya kigeni Allium Sativum ni moja kati ya zao bora lenye manufaa mengi kwa matumizi ya kila siku kwa maisha ya mwanadamu, kiafya, Kitabibu na kwa ajili ya kutengeneza au kuchanganyia katika dawa tofauti. Pia ni kiungo mahusui katika mambo ya mapishi.

Zipo aina tisa za vitunguu swaumu ambazo hulimwa hapaduniani katika maeneo mbalimbali.

Aina za vitunguu saumu maarufu kwa matumizi ya kawaida ni tatu,

1. SOFT NECK - ni nyeupe huzaa kwa muda mfupi.

2. SILVER SKIN - vina rangi ya silver vikikaushwa vinaweza kukaa hadi mwaka mmoja.

3. ANTICHOKE - vina rangi nyekundu kwa mbali.

katika nchi yetu ya tanzania vinapatikana vitunguu swaumu ya aina tatu

1. Kitunguu saumu chenye mafuta makali.

2. Kitunguu saumu chenye madini ya protini

3. kitunguu saumu chenye madini, protini na mafuta mepesi. Hapa Tanzania tunalima aina hii ya tatu.

NAMNA YA KULIMA

Kitunguu hiki hulimwa katika maeneo yenye baridi uwanda wa jua hafifu, mvua za wastani na joto hafifu, aridhi iwe nyeusi yenye rutuba na mfinyanzi, kusiwe na upepo mkali au ukungu mwingi.

Hulimwa kwa kuandaa kitaluna kupandikizwa baada ya miche kufikia urefu wa inchi 6-14, hupandwa kwa mstari na mche hadi mche ni nchi 3-4 na mstari kwa mstari ni nchi 12.

Kwa kifupi kitunguu swaumu ni kati ya zao gumu sana kulilima kwani hustawi katika maeneo machache sana hapa duniani. Kwa hapa tanzania hustawi katika Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Mbulu, Hanang na babati kidogo, pia kidogo mkoa wa kilimanjaro na kwa eneo lolote ambalo hali inaendana na maeneo tajwa hapo juu.

Kwa Mkoa wa Morogoro vitunguu saumu vinalimwa maeneo ya Mgeta,Wilaya ya Mvomero.

UANDAAJI WA SHAMBA

Tifua udongo kidogo kisha ufanye hallowing ili kurahisisha upandaji na ukaaji wa mimea tu. Tengeneza tuta za mita 1 hadi 1.5, upana mita 10 urefu. Kwa upande wa mbolea Inashauliwa utumie WINNER

UPANDIKIZAJI

Vibanguliwe vipandwe kwa kuelekezea mizizi chini na kina cha wastani 2.5 inchi, mbolea ya samadi hushauriwa zaidi kutumika, Huvunwa baada ya miezi 4 -6 kulingana na hali ya hewa na aina ya mbegu iliyotumika.

SPACING/ MUACHANO WA MBEGU NA MBEGU

Mstari hadi mstari ni inchi 8 na mmea hadi mmea ni inchi 6 yaani (8*6)inchi

KIWANGO CHA MBEGU

Kiwango cha mbegu ni kilo 200 - 300 kwa heka moja

MAVUNO

Ni tani 5 -6 kwa heka moja

UANDAAJI WA MBEGU

Kitunguu swaumu hupandwa "BULB" na sio mbegu kama vitunguu maji. Ni ile Punje ambayo Imekuwa na kukomaa vizuri na isyoathiliwa na magonjwa

MAGONJWA

1. Vitunguu saumu havishambuliwi na magonjwa kama ilivyo mazao mengine.

2. Mimea ikianza kutoa maua, yaache yawe marefu hadi yajikunje kisha utayakata ili kuongeza uzalishaji.

Wadudu wasumbufu ni THRIPS na ukungu upande wa magojwa.

Kwa upande wa ukungu anza na RIDOMILL GOLD upulizie mara nne kisha malizia na score kwa ajili ya Thrips tumia ACTARA au MATCH.

Hushambuliwa na magonjwa kuanzia wiki ya Tatu hadi ya saba, Tumia madwa ya kupuliza yatumikayo kwa nyanya na vitunguu vya kawaida.

SOKO

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika soko la Kariakoo kilo moja ni inakadiriwa kuwa kati ya Tsh.4000 hadi 6000. Ila kwa ujumla ni bidhaa ambayo inahitajika kwa wingi ndani na nje ya nchi.

 

No comments:

Post a Comment