Mwenyekiti wa Morogoro Press Club,Nickson Mkilanya,akiwasilisha taarifa kwa Ujumbe wa Ubalozi wa Sweden uliotembelea MoroPC
UBALOZI WA SWEDEN WATEMBELEA MOROGORO PRESS CLUB, WATOA PONGEZI
UJUMBE ubalozi wa Sweden nchini Tanzania umefanya ziara katika Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro na kupokea taarifa ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Waandishi wa habari katika mkoani humo.
Ziara hiyo imelenga zaidi kutambua jinsi Klabu za waandishi wa habari ambazo zinapokea ufadhili kutoka Sweden kupitia Umoja Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ambapo Morogoro Press Club ni miongoni mwa wanufaika na ufadhili huo kwa kuwa ni mwanachama hai wa UTPC.
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club,Nickson Mkilanya alitoa taarifa za kazi mbalimbali zilizofanywa na Klabu yake kwa Maafisa kutoka ubalozi wa Sweden ikiwemo utekelezaji wa falsafa ya Good To Great unaochagizwa na Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) kwamba, Morogoro Press Club ni miongoni Klabu 28 zilizopo hapa nchini.
Mkilanya katika taarifa yake amebainisha mafanikio hayo ni pamoja na uboreshaji wa mifumo ya fedha na utawala,demokrasia na utawala bora,usalama wa waandishi wa habari pamoja na uandishi wa habari zenye masilahi ya umma,zilizoleta mabadiliko katika jamii (story of change).
Aidha,uongozi wa Morogoro Press Club ulibainisha jinsi wanachama wake wanavyoibua changamoto zilizopo katika jamii zilizopo pembezoni.Habari hizo ziliandaliwa na mmoja wa wanachama wa Morogoro Press Club, Jacob Sonyo zilirushwa na kituo cha Ayo Tv habari hizo zilileta mabadiliko,wadau mbalimbali walijitokeza na kutoa msaada kwao.zinapatikana kupitia; https://youtu.be/moEfXOPc8ZQ?si=0mMksJ7KjaPdiTOp,https://youtu.be/Ltpct4ft4uo?si=u_XDb9Py1AEK3WzC ,https://youtu.be/vnOXgKtHRP8?si=OZx1-BkJCeoxfZHj, https://youtu.be/xuho6LfYHcE?si=hD3Kuhu2rDNntyCG
picha ya pamoja kati ya ujumbe wa Ubalozi wa Sweden na Uongozi wa Morogoro Press Club mara mara ya kufanya mazungumzo ya pamoja wakichangiza falsafa ya 'from Good To Great'waliwa na nyuso za furaha.Miongoni mwa habari hizo ni Kijana mmoja mkazi wa Mlimba,Wilaya ya Kilombero mwenye ulemavu wa viungo ambaye anatumia miguu yake badala ya mikono katika kujihudumia kula na hata masomo yake darasani kuandika na kuchora lakini kwa sababu ya familia yake ina kipato cha chini alijikuta akikabiliwa na changamoto katika safari na ndoto zake katika elimu.Baada ya jamii habari hiyo kuchapishwa ilileta mabadiliko kwa jamii kuguswa na kutoa msaada kwake.
Mbali na hayo,pia Ujumbe wa ubalozi wa Sweden,uliambatana na Mkuu wa Program kutoka UTPC,Severin Mapunda waliguswa na kuipongeza Waandishi wa Habari wa Morogoro kwa kuibua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii,baada ya kuoneshwa video ya mama mmoja (39) mkazi wa Manispaa ya Morogoro ambayo amezaa watoto 13 na kutelekezwa na mumewe.
Maafisa wa Ubalozi wa Sweden wakifurahia jambo walipotembelea Morogoro Press ClubUjumbe wa ubalozi wa Sweden hapa nchini uliotembelea Morogoro Press Club ni Stephen Chimalo,Samwel Saigilu na Tove Lindgen Jansson,wameipongeza na wameridhishwa na kazi nzuri zinazofanywa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro.
Mmoja wa Maafisa wa ubalozi wa Sweden,Stephen Chimalo amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mpango kazi wa kutembelea baadhi ya Klabu za waandishi wa habari ili kuangalia ufanisi katika shughuli zao.
No comments:
Post a Comment