Breaking News

Feb 25, 2021

SHIRIKISHO LA MIFUKO YA JAMII,TSSA YADHAMIRIA KUFUFUA KIWANJA CHA MOROGORO CANVAS

 



WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU SERA,BUNGE,KAZI,AJIR NA WATU WENYE ULEMAVU,JENISTA MHAGAMA AKISISITIZA JAMBO WAKATI AKIFANYA MAJUMUISHO YA KUTEMBELEA KIWANJA CHA MOROGORO CANVAS AMBAPO SHIRIKISHO LA MIFUKO YA JAMII(PSSA) WAMEDHAMIRIA KUFUFUA KIWANDA HICHO,

SHIRIKISHO LA MIFUKO YA JAMII,TSSA YADHAMIRIA KUFUFUA KIWANJA CHA MOROGORO CANVAS

Na Thadei Hafigwa

SHIRIKA la ufatifi wa viwanda nchini (TIRDO) limepewa zabuni ya kutazama namna ya kuwekeza kwenye viwanda vya sekta ya nguo na ngozi na kiwanda cha Morogoro Canvas ambacho kimesimamisha uzalishaji wake toka mwaka 2016 wapo katika hatua za mwisho kwa kufanya upembezi yakinifu ili kuona mradi huo unavyoweza kuwa na tija.

 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Jamii nchini (TSSA), Meshack Bandawe amebainisha hayo mbele ya mbele ya Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kuongeza kuwa TSSA wamefikia hatua hiyo baada ya kudhamiria kuwekeza katika kiwanja hicho kitakachofufua matumaini ya wakazi wa morogoro kupata ajira.

Bandawe alisema mwaka 2016 Rais wa Tanzania John akiwa jijini Arusha wakati akizindua Majengo ya NSSF na PPF alitoa wito na maagizo kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuangalia namna ya kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini hivyo baada ya maagizo hayo mifuko ilianza utekelezaji huo mara moja.

“Wakati tafiti na pembuzi yakinifu zikiendelea kufanyika katika kiwanda cha kutengeneza maturubai cha Canvas cha mkoani Morogoro, Shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii nchini(TSSA) imedhamiria kufufua kiwanda hicho kwa kuwekeza”Alisema.

Alisema kuwa,moja ya maeneo ambayo ilitizama kwa umoja wao ni kuangalia namna ya kuwekeza kwenye viwanda vya sekta ya nguo na ngozi na kiwanda cha Morogoro Canvas ambapo wakati huo kilikuwa tayari kimesimamisha uzalishaji wake na hapo walianza kuchukua hatua ya kufanya upembezi yakinifu ili kuona mradi huo unavyoweza kuwa na tija na shirika la Utafiti wa viwanda nchini (TIRDO) ulisaidia kufanya kazi hiyo.

KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA MIFUKO YA JAMII(TSSA),MESHACK BANDAWE  ( KUSHOTO) AKIFUATILIA KWA KARIBU HOTUBA YA WAZIRI JENISTA MHAGAMA

Katibu mkuu huyo alisema kuwa baada ya tafiti kufanyika TIRDO iliwasilisha taarifa yao na kueleza kuwa uwekezaji unaoweza kufanyika katika kiwanda hicho utakuwa na tija kwa mifuko na taifa kwa ujumla.

“Ilipofika tarehe 27 mwezi Januari mwaka huu serikali ilitoa idhini kupitia ofisi ya msajili wa hazina kwamba mifuko inaweza kuendelea na uwekezaji katika kiwanda hiki,kazi inayofuata baada ya hapo ni kujadili uzalishaji unavyoweza kuanza tena na tumechukua  na kuipa kazi tena TIRDO ili kuuwisha taarifa yake ili kufuatana na mazingira ya sasa,”alisema Bandawe.

Alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaongeza mnyororo wa thamani kwa zao la Pamba ambalo ndilo malighafi inayotumika katika kuzalisha bidhaa zinazopatikama kwenye kiwanda hicho.

Akizungumza akiwa katika kiwanda cha Canvas mara baada ya kutembelea viwanda viwili vya Nguli hill cha Nyama, na cha Canvas cha kutengenezwa Maturubai,Sare za majeshi,Waziri Mhagama alizitaka menejimenti za viwanda hivyo pindi vikianza uzalishaji Mara baada ya kufufuliwa kwake kuhakikisha wanaweka mikakati ya Kufahamu Ajira rasmi na zile zisizo rasmi kwa kuwepo kwa mikataba kwa wafanyakazi wake.

"Suala la Ajira Serikali ya awamu ya tano ni kipaumbele Sana,zile za moja kwa Moja na zisizo za moja kwa Moja, hakikisheni hivi viwanda havifi tena jipangeni na kuweka mikakati Bora,"alisema waziri Mhagama.

Aidha Waziri huyo alipongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania (TSSA) ya kufuata kiwanda Cha Canvas ambacho linatarajiwa kuanza kufanyakazi mwezi Juni ama Julai mwaka huu na kueleza kuajiri watu Kati ya 500 Hadi 800.

Pia alisema kuna kazi ya kumaliza mazungumzo na Banki ya CRDB ambayo ilikuwa ikikidai kiwanda hicho shilingi 18.9 bilioni yamekuwa yenye kuleta mafanikio, na kuwataka kumaliza mazungumzo hayo haraka na yakikamilika mapema ndani ya mwezi Februari na ikikamilika yatatoa nafasi na fursa kwa mifuko kijupanga.

No comments:

Post a Comment