NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI,PAULINE GEKUL AKIHUTUBIA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHAMAKWEZA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE
SERIKALI
YATOA MIL 700 UJENZI WA LAMBO,KUTATUA MIGOGORO WAKULIMA NA WAFUGAJI CHALINZE
NA
VICTOR MASANGU, CHALINZE
KUFUATIA kuwepo kwa wimbi la mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii ya
wakulima na wafugaji katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo halmashauri ya
Chalinze na kusababisha hali ya uvunjifu wa amani serikali ya awamu ya
tano imekuja na mpango wa kukomesha hali hiyo ambapo imedhamiria kutatua
migogoro ipatayo 40 ambayo tayari imekabidhiwa katika Wizara
husika.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Pauline Gekul wakati
wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea mradi wa lambo kubwa la
kunyweshea mifugo pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi
katika vijiji vitatu vya vya Chamakweza, Ruvu darajani na kijiji cha
Kitonga vilivyopo katika halmashauri ya Chalinze.
Aidha, Naibu
Waziri huyo aliwataka jamii ya wafugaji na wakulima wote katika maeneo mbali
mbali ya halmashauri ya Chalinze kwa sasa kuwa watulivu na wahakikishe
wanazingatia sheria na taratibu zote za nchi ikiwemo kuheshimiana wakati
serikali inaendelea na juhudi za makusudi katika kulitaua jambo hilo la mgogoro
uliokuwepo ili amani iweze kurejea.
“Nimepokea katika Wizara yangu migogoro ipatayo 40 na hii inahusiana na mambo haya haya wa migogoro katika ya wakulima na wafugaji na vijiji hivi vya chamakweza pamoja na pingo na maeneo mengine ni moja ya sehemu ambayo na yenyewe ipo katika mvutano huu lakini mimi nina waahidi kulimaziza suala hilo na uzuri limeshafika katika mamlaka zinazohusika wala sio kwa Mkuu wa Mkoa tena.,”alifafafanua Naibu Waziri huyo.BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA WAFUGAJI CHAMAKWEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE WAKIFUATILIA KWA KARIBU HOTUBA ZA VIONGOZI WA SERIKALI WALIPOTEMBELEA KIJIJI HICHO KATIKA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YAO.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo amebainisha lengo la
serikali ni kuhakikisha inazifuatilia fedha ambazo zimetolewa kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya maendeleo ili kujionea kama ipo katika kiwango
kinachotakiwa na kuwataka wafugaji na wakulima kumaliza kabisa migogoro
na mapigano yao na kuachana na kufanyiana vitendo vya ubaguzi.
Mmoja wa
wa wafugaji akisoma tamko lao ambalo wameliandaa mbele ya
Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi kwa niaba ya wenzake amebainisha kwamba
kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi ya wakulima kufanya uvamizi katika
maeneo ya marisho na kuamua kuyauza kinyemela kwa watu kutoka maeneo mbali
mbali.
Naye Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa katika jambo ambalo wamekuwa
wakilipigia kelele kwa kipindi kirefu ni mradi wa ujenzi wa lambo hilo
kwa ajili ya mifugo na kwamba ameipongeza serikali ya awamu tano kwa
kutoa kiasi cha shilingi milioni 700.
“Kwa kweli
kwa upande wangu mimi kama Mbunge wa Jimbo la Chalinze nipende kumshukuru Rais
wetu wa wamau wa tano kwa kuweza kututhamani sisi wananchi kukubali kutoa kiasi
cha shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu wa bwawa kubwa katika
kijiji hiki cha chamakweza na litaweza kuwa mkombozi mkubwa wa mifugo
yetu,”alisema Mbunge Huyo.
Pia alisema
kwamba ni kweli kumekuwepo kwa changamoto kubwa kwa wakulima na wafugaji katika
baadhi ya maeneo ya vijiji hasa katika eneo hilo la wananchi
wa vijiji vya Chamakweza na pingo lakini anashukuru viongozi mbali mbali
wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani pamoja na Naibu waziri wa mifugo na
uvuvi kufanya ziara maalumu kwa ajili ya kwenda kutafuta ufumbuzi.
Halmashauri ya Chalinzie Iliyopo Wilayani Bagamoyo imekuwa ikikabiliwa na chanagmoto kubwa
katika baadhi ya vijiji vyake kuwepo kwa migogoro kila kukicha na mapigano kati
ya wakulima na wafugaji kutokana na kugombania maeneo ya mipaka ya ardhi
hivyo na kusababisha vurugu hivyo jitihada ambazo zimefanywa na serikai
ya awamu ya tano zitaweza kuleta matokeo chanya ya kumaliza vurugu hizo
No comments:
Post a Comment