WAZIRI
KALEMANI AMPA MKANDARASI SIKU 10 KUKAMILISHA UJENZI ‘KIPOZA’ UMEME KILOMBERO
Na Lilian Kasenene,
Morogoro.
WAZIRI wa
Nishati, Dk Medard Kalemani ameonyesha kukasilishwa na namna ucheleweshwaji wa
Ujenzi wa kituo cha kupoza umeme unaotoka kidatu kwenda wilaya za
Ulanga,Kilombero na Malinyi kinachojengwa mjini Ifakara na kutoa siku kumi kwa
mkandarasi wa Ujenzi huo kampuni ya AEE Power kuanza Mara Moja ili uweze
kukamilika kwa wakati.
Dk Kalemani, alitoa agizo
hilo jana, mjini Ifakara wilayani Kilombero alipotembelea na kukagua eneo la
mradi kinapojengwa kituo hicho cha kupooza umeme kinachojengwa kwa gharama ya
shilingi 23 bilioni hadi kukamilika kwake
zilizotolewa na serikali.
“Kwa muda mrefu wilaya hizi zimekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara hivyo mradi huo utakuwa mwarobaini wa tatizo la kukatika kwa umeme maeneo haya ya Ifakara,Malinyi na Ulanga tatizo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi na kutaka wananchi wapate umeme wa uhakika,”alisema Waziri Dk Kalemani.
WAZIRI WA NISHATI,DK MEDARD KALEMANI AKISISITIZA JAMBO WAKATI APOTEMBELEA UJENZI WA MRADI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME KILOMBERO,MKOANI MOROGORO,AMBAPO AMEKERWA NA HALI YA UCHELEWESHWAJI WA UJENZI WA MRADI HUO(PICHA NA LILIAN LUCAS)Dk Kalemani alimtaka
mkandarasi kuleta vifaa vya kutosha
pamoja na wataalam wa kutosha ili mradi ukamilike kwa wakati.
Aidha alisema alipata
taarifa ya kutoelewana kati ya mkandarasi na msimamizi mwelekeze wa mradi huo
na kuwataka kuacha mara moja malumbano yanayoendelea Kati yao na kuwa malumbano
yao yasiwaumize wananchi kwani wanahitaji umeme kwa haraka na malumbano yao
hayana tija kwa sasa.
Alisema kwa sasa wananchi
wanahitaji umeme kuliko wakati mwingine wowote ni vyema wataalamu na
wakandarasi wanaopewa miradi ya umeme kuhakikisha wanafannya kazi na kujenga
kwa wakati maeneo yote yanayohitajika kujengwa na kuwataka meneja wa shirika la
umeme Tanzania(Tanesco) wa wilaya, mikoa na wale wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA)
kusimamia kikamilifu.
Dk Kaleman pia ameitaka
bodi ya wakala wa Nishati vijijini REA kuweka kambi kwenye mradi huo na kuanza kazi mara moja huku akiitaka bodi
hiyo kutomuongezea muda mkandarasi bali kumsimamie mradi ili ukamilike ndani ya
wakati kwa mujibu wa mkataba.
Awali, akielezea maendeleo
ya mradi huo, meneja mradi kutoka Tanesco Didas Lyamuya alisema kuwa mpaka sasa
mkandarasi yuko kwenye zoezi la ujazaji wa kifusi na vifaa vimeshaagizwa na
matarajio Transfoma kubwa kufika Septemba mwaka huu.
Akieleza baadhi ya
Changamoto iliyopo eneo la Mradi ni tafsiri ya kutoelewana ya kiwango cha
Udongo namna gani kijazwe ili thamani ya fedha iweze kuonekana.
Ujenzi wa kituo hicho
kikubwa cha umeme kitakuwa kina uwezo wa kuingiza Voteji 220 na kutoa voteji 33
kwa wananchi na hiyo itakuwa mkombozi wa tatizo sugu kukatika kwa umeme huo
mara kwa mara kwenye maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment