Na Natharine Ugulumo
WATAFITI
duniani wanaendelea na ’ kupanoa bongo’ dhidi ya kutafuta ufumbuzi wa homa ya
mapafu covid 19,ugonjwa ambao unaendelea kuisumbua dunia.
Baadhi ya watu
walikuwa na hisia ya kuwa kuenea kwa Covid 19 inategemeana na hali ya hewa joto
au baridi,lakini watafiti na wataalamu nawaeleza kuwa Unaweza kupata COVID-19 licha ya hali ya hewa
ya jua au joto jingi iliyopo katika eneo husika.
Nchi zilizo na hali ya
hewa ya joto zimeripoti visa vya COVID-19. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa njia
bora ya kujilinda dhidi ya COVID-19 ni kukaa mbali na wengine na kusafisha
mikono yako mara kwa mara na ipasavyo.
Nchini Tanzania
kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kipindi cha
covid 19 imeweza kufanikiwa kutoa elimu kwa wananchi kuendelea kuchukua
tahadhali ya kutosha kwa kuzingatia misingi ya afya kwa kunawa maji tiririka
mara kwa mara si kwa kupambana na covid 19 pekee bali pia kujikinga na magonjwa
ya mripuko ikiwemo homa ya matumbo,kuhara na kutapika.
Pia, wananchi kwa
imani zao walikesha kuomba Mungu kwa sala na dua kwenye misikiti na
makanisa,hali hiyo imesaidia Tanzania kutokuwa na athari kubwa ya covid 19

No comments:
Post a Comment