WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWAELIMISHA JAMII JUU YA COVID 19
Na Lilian Lucas
MGANGA wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro amewaeleza waandishi wa habari kwamba wanapaswa kutumia vema kalamu zao vema ili kuepuka kanganyiko kwa wananchi hasa kuna dhana kwamba watu wenye umri mkubwa kupata maambukizi ya covid 19.
Dk.Kusirye Ukio alisema
waandishi wa habari wanategemewa sana na jamii hivyo wanapotimiza wajibu wao wa
kitaaluma ni vema kalamu zao zisitumike kuwatisha jamii dhidi ya covid hasa na badala yake kuwaelimisha vema kuzingatia
kanuni za afya.
Ukio alisema kuwa
waandishi wanapaswa kuwasiliana na mamlaka husika hasa wanapoandika habari zinazohusiana
na afya ili matumizi sahihi ya maneno yanayohusu afya ya mwanadamu ili kuepuka
mkanganyiko wa uelewa kwa jamii.
Aidha,Alisema kuwa,
ugonjwa wa covid 19 una historia yake lakini, taaluma ya habari isitumike
katika kuwapotosha jamii na badala yake iwaelimishe Jamii kwa kuzingatia miongozo
inayotolewa na Wizara ya afya.

No comments:
Post a Comment