RC
PWANI AKIZINDUA MV KILINDONI WILAYANI MAFYA
NA
VICTOR MASANGU, MAFIA
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amepokea kivuko
kipya kilichopewa jina la Mv Kilindoni – Hapa kazi tu, kilichogharimu kiasi cha
shilingi bilioni 5.3 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa lengo la kuwaondolea wananchi wa Wilaya ya
Mafia adha ya usafiri ambayo walikuwa wanakabiliana nayo.
Mhandisi Ndikilo, amepokea kivuko hicho kwa
niaba ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi, Mh. Mhandisi, Leonard Chamuriho,
wakati wa sherehe ambazo zilifanyika katika visiwa vilivyopo
Wilayani Mafia na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali. Wakuu
wa taasisi mbali mbali pamoja na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi
sambamba na wananchi.
Mkuu huyo, alisema kwamba, kivuko hicho ni moja ya ahadi ambazo zilitolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Mafia na maeneo mengine waweze kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya usafiri wa majini ambao ulikuwa unawasumbua kwa muda mrefu.
MKUU WA MKOA WA PWANI,MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO CHA MV KILINDONI-MAFYA Pia, alifafanua kwamba, kivuko hicho ambacho kina uwezo wa
kubeba abiria wapatao 200 pamoja na tani 100 za mizigo kinatarajia kuanza
kufanya safari zake rasmi Februari 3,2021 ambapo kitakuwa kinawabeba wananchi
mbali mbali kutoka eneo la Nyamisati na kuelekea katika eneo la kilindoni
Wilayani Mafia na kwamba ujenzi wa kivuko huo umefanywa na Songoro Marine
Trasport Boatyard LTD ya Mwanza.
“Kivuko hiki kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3 na
kwamba fedha hizi zimetolewa na Rais wetu Mpendwa hivyo tunampongeza sana kwa
ahadi yake na kwamba hapo awali wananchi wa mafia bado walikuwa na changamoto
ya usafiri wa majini japo kuna kivuko kingine kilikuwepo cha mtu binafsi ambacho
nacho kimeweza kusaidia sana wananchi na hiki cha serikali kina uwezo wa kubeba
abiria 200 na tani 100 za mizigo,”alifafanua Ndikilo.
SEHEMU YA MUONEKANO WA MV KILINDONI-MAFYA,KILICHOZINDULIWA NA MKUU WA MKOA WA PWANI,MHANDISI EVARIST NDIKILO.
Katika hatua nyingine, Ndikilo alisema kwamba kivuko hicho pia kitaweza kufungua fursa za kiuchumi kutokana na wananchi wa Mafia kuweza kuendesha shughuli zao mbali mbali za uzalishaji mali na biashara na kuwahimiza waweze kuwa walinzi wazuri katika kukitunza kivuko hicho ambacho walikuwa wakikisubiria kwa shauka kubwa.
“Asante sana Mh. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kwa kuweza kutekeleza ahadi yako ya kuleta kivuko hicho ambacho
kitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia na kufungua
zaidi fursa za wananchi wengine katika kufanya biashara,”alisema Ndikilo
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM),
Mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno pia ametoa pongezi zake za dhati kwa Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kwa kuweza kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa
ajili ya kivuko hicho ambacho ameeleza kuwa kitaweza kuwa ni moja ya kuleta
chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani na maeneo
mengine.
Nao, baadhi ya wananchi Wilayani Mafia, ambao wamehudhuria
katika sherehe hizo, walisema kwamba, hapo awali walikuwa wanakabiliwa na
changamoto katika suala zima la usafiri, hivyo kukamilika kwa kivuko hicho
kitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanya shughuli zao na kuleta
maendeleo.
“Kwa kweli sisi kama wananchi wa ya Mafia tunapoa shukrani zetu
kwa Rais wetu Mpwendwa kwa kuweza kutujali na kutuletea kivuki hiki ambacho
kinajulikana Mv Kilindoni, na kwamba kitakuwa ni moja ya kutataua changamoto za
usafiri na kitarahisha zaidi utaekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku na
kukuza uchumi zaidi.”walisema wananchi hao.
Wananchi wa Wilayani Mafia Mkoa Pwani wamekuwa wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya siku nyingi, adha ya usafiri wa majini hivyo kukamilika kwa
kivuko hicho cha Mv kilindoni – Hapa kazi tu, kutaweza kuleta mabadiliko
makubwa hasa katika Nyanja mbali mbali za kukuza uchumi, pamoja na wananchi
kupata fursa ya kuendesha biashara zao mbali mbali ikiwemo kuwavutia
wawekezaji.



No comments:
Post a Comment