Breaking News

Feb 1, 2021

KATIBU TAWALA BAGAMOYO AKERWA TABIA YA ‘WIZI’ WA DAWA KWA WATUMISHI WA AFYA


KATIBU TAWALA BAGAMOYO,KASILDA MGENI

KATIBU TAWALA BAGAMOYO AKERWA NA ‘WIZI’ WA DAWA

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

SERIKALI wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, imekemea vikali tabia ya  baadhi ya watumishi  wa afya kuamua kukiuka viapo vya kazi zao kwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa madawa na kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hali  ambayo ni  kinyume  kabisa na maadili ya utekelezaji wa majukumu yao.

Kauli hiyo, imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea katika kituo cha afya Kerege kwa ajili ya kuweza kujionea huduma mbali mbali zinazotolewa  na watumishi hao wa afya pamoja na kusikiliza changamoto zilizopo kwa lengo la kuzitafutia ufumbuzi.

“Nimeweza kutembelea katika kituo hiki cha afya Kerege niweze kuzungumza na watumishi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuweza kujionea shughuli mbali mbali ambazo zinafanyika ikiwa ni kuona namna ya kuweza kuboresha sekta ya afya ili wananchi waweze kupata fursa ya kupata matibabu yanayostahili na hii itapunguza kwa kiwango kikubwa malalamiko ya wananchi,”alisema Mgeni.

Aidha, Mgeni aliongeza kuwa, lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuboresha huduma ya afya kwa wananchi na kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili kwa kuweka mipango madhubuti ya kuongeza wataalamu zaidi wa afya ikiwemo kujenga zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuboresha zaidi huduma ya matibabu kwa wananchi.

Pia,Katibu huyo, alisema kuwa,ameakua kufanya ziara zake za kikazi katika maeneo mbali mbali ya zahanati, vituo vya afya pamoja na Hospitali katika Wilaya hiyo ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuibua changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wauguzi, madaktari pamoja na  watumishi  wa afya  na kuzisikiliza changamoto ili kuzifanyia kazi.

Katibu Tawala huyo, alisema kwamba inasikitisha sana kuona Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli akitoa  fedha nyingi kwa ajili kuboresha huduma katika sekta ya afya lakini bado kunakuwepo na baadhi ya wananchi kutoa malalamiko juu ya upatikanaji wa huduma ya afya.

Kadhalika, alibanisha kuwa malalamiko mengi ambayo yanatolewa na  baadhi ya wananchi ni kuwepo kwa kucheleweshewa huduma ya matibabu kutokana na baadhi ya watumishi kuomba rushwa na wengine kuwa na lugha ambayo sio rafiki na kutoa huduma kwa upendeleo hali hiyo ambayo inapelekea kuibuka kwa malalamiko hayo.

Katika hatua nyingine, amesikitishwa na tatizo la wizi wa madawa katika vituo hivyo vya afya ambapo amedai kumekuwa na baadhi ya watumishi kuamua kuiba madawa na kwenda kuyauza katika maduka yao binafsi kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi na kupeleeka ukosefu wa madawa kwa wananchi hao.

No comments:

Post a Comment