NA VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa
Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amelitaka jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani kuhakikisha kwamba linaweka mikakati madhubuti kwa ajili ya
kuthibiti wimbi la uharifu pamoja na kukomoshe matumizi ya madawa ya kulevya
ikiwemo bangi pamoja na unywaji wa pombe haramu ya gongo ambayo ina madhara
makubwa kwa afya ya binadamu.
Ndikilo, ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza na askari
wa jeshi la polisi kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe
maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuuaga mwaka wa 2020 na kuukaribisha mwaka
mpya wa 2021, pamoja na kuweza kupanga mikakati ya kulinda hali ya ulinzi
na amani pamoja na kujadili changamoto zilizopo kwa askari polisi ili kuweza
kuzitafutia ufumbuzi.
Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama
mkoa, alisema kuwa kumekuwepo kwa baadhi ya maeneo bado kuna baadhi ya watu
wanajichukulia sheria mikononi na kusababisha uvinjifu wa amani hivyo alimuagiza
Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba analilisimamia suala hili
kikamilifu na kuongeza zaidi doria katika maeneo mbali mbali lengo ikiwa ni
kuimarisha hali ya ulinzia kwa wananchi.
“Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Pwani nashukuru sana kupata mwaliko
katika sehehe hizi ambazo zimeandaliwa na jeshi la polisi lakini kitu kikubwa
ninachowaomba ni lazima sasa kuweka mipango mizuri ya kutekeleza wajibu wetu
ipasavyo maana katika baadhi ya maeneo bado kuna watu wanaendelea kufanya
vitendo vya uharifu hivyo ni lazima kuwabaini wale wote ambao wanahatarisha
uvunjifu wa amani na wakamatwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria,”alisema
Ndikilo.
Aidha, Ndikilo, alibainisha kwamba, anachukizwa sana kuona bado
kuna baadhi ya wananchi wanandelea kutumia pombe aina ya kongo ambayo ni haramu,
hivyo ameliagiza jeshi hilo kufanya msako mkali kwa ajili ya kuwakamata wale wote
ambao watakutwa wanatumia pombe hiyo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na
taratibu za nchi.
Kadhalika, alisema kuwa serikali ya awamu ya tano, lengo lake
kubwa ni kuhakikisha kwamba inaweka misingi imara katika kulinda nchi yake
katika sehemu mbalimbali, hivyo, askari wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya dola waendelee kufanya doria za mara kwa mara katika mipaka
ili kuthibiti waharifu na watu wengine wasiingie nchini kinyemela na kuja
kufanya uharifu.
“Kumekuwepo na wimbi la wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini
kinyemela pasipo kuzingatia sheria na taratibu, naliagiza jeshi la polisi
pamoja na maafisa mbalimbali wa ulinzi kuhakikisha wanalinda mipaka ya
nchi ya sehemu nyingine ambazo baadhi ya raia wa kigeni wanatumia njia hizo
katika kupita na kuingia nchini hasa katika maeneo ya bandari bubu kama vile
maneo ya Wilayani Bagamoyo,”aliongeza Ndikilo.
Pia, katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa alilipongeza jeshi
la polisi Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuweka mikakati ya kupunguza ajali za
barabarani kwa kiwango kikubwa na kuwataka watumiaji wa vyombo vya
usafiri kuhakikisha kwamba wanazingatia sheria zote za barabarani ili kuepukana
na ajali ambazo zinapelekea watu kupoteza maisha yao na wengine kupata ulemavu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa
alimahidi Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani, kuzishughulikia changamoto mbalimbali
zilizopo na kwamba ataendelea zaidi kulivalia njuga suala la wimbi la uharifu
kwa lengo la kudumisha hali ya ulinzia na usalama.

No comments:
Post a Comment