WADAU WA KILIMO WATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO WAKULIMA WADOGOWADOGO
Thadei Hafigwa
MADIWANI na
wadau wa Kilimo wametakiwa kuwa na mtazamo wa haki za binadamu na kushiriki
katika mchakato wa maendeleo kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,miongozo
ya tamisemi,fursa na vikwazo na uundaji wa bajeti ikiwa ni njia ya kuwasaidia
wakulima wadogowadogo kupata mafanikio chanja katika shughuli zao za Kilimo.
Wakiwasilisha mada kwa
nyakati tofauti,katika mafunzo wa madiwani na wadau wa kilimo wilaya ya Mvomero
mkoa wa Morogoro,Venance Mlali na Dk.Albinie Marcossy walieleza kwamba nafasi
ya madiwani ni kubwa katika kutatua changamoto zinazowakabili wakulima katika
kupata maendeleo kwenye sekta ya kilimo.
Venance Mlali wa Asasi ya
Mafiga women alisema kuwa ili mkulima mdogomdogo aweze kupata haki yake hapana
budi kuzingatia malengo ya kimataifa kwa kuzingatia lengo namba moja na namba
mbili ambapo imeweka bayana haki za binadamu kushiriki kwenye mchakato ya
maendeleo kwa kuzingatia katiba ya nchi.
Zao la ndizi ni moja kati ya mazao yanayozalishwa na wakulima wadogowadogo nchini Tanzania.
“Kiini cha yote ni mfumo wa
uwajibikaji ili kupata matokeo chanja kwenye sekta ya kilimo kujua bajeti za
halmashauri ambao ndio msingi wa kufanikisha katika kukabiliana na umaskini na
njaa”Alisema.
Kwa upande wake,Dk.Albinie Marcossy alisema kuwa mpango
wa maendeleo ya taifa na program ya miaka mitano ya kuendeleza sekta ya kilimo
awamu ya pili ambapo maeneo mahususi katika mfumo wa utekelezaji na ufuatiliaji
kuanzia ngazi ya kijiji hadi ofisi ya waziri mkuu umebebwa na msingi wa
uwajibikaji wa jamii,viongozi wa umma wakiwemo madiwani.
Mafunzo hayo kwa madiwani yameandaliwa na mtandao wa wakulima wadogowadogo Tanzania(MVIWATA) kwa kushirikiana na mtandao wa wakulima Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika(ESAFF)
Irene Liborius,Afisa mradi wa ESAFF amesema kuwa madiwani katika masuala ya uwajibikaji na ushiriki wa wakulima katika sekta ya kilimo ni suala mtambuka katika utekelezwaji nchini Tanzania kwa kuzingatia mipango ya kimataifa na Afrika (CAADP) kuhusu usalama wa chakula.Aidha,Mwakilishi kutoka Mtandao wa wakulima wadogowadogo
Tanzania (MVIWATA), Theodora Pius alisema kuwa
Mviwata imekuwa ikiwasogezea wakulima wadogowadogo huduma kwa msingi ya
ushawishi na utetezi kwa kufanikiwa kujenga soko la nyandira,kutoa mafunzo kwa
wakulima ili kuendesha kilimo chenye tija.
No comments:
Post a Comment