Breaking News

Dec 24, 2020

VIJANA WANENA USHIRIKI WA0 KAMPENI JANGA LA CORONA MOROGORO

 

MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA KINARA YOUTH EVOLUTION,CHARLES SALU


VIJANA WANENA USHIRIKI WA0 KAMPENI JANGA LA CORONA MOROGORO

 Na Daud Julian

SHIRIKA lisiyo la kiserikali la Kinara manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa mashirika yanayojishughulisha na maendeleo ya vijana,limeshiriki kikamilifu katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kipindi cha covid 19 kwa kugawa ndoo na sabuni za kutakasa mikono.

Charles Salu, mkurugenzi Mtendaji wa Kinara youth evolution akiongea na blog ya moropc kuwa shirika lake limeshiriki kikamlifu katika kampeni wakati wa corona,kampeni iliyojulikana ‘Kinara dhidi ya corona’  

Salu alisema kuwa daima wamekuwa  furaha baada ya kutoa ndoo kubwa za kunawa mikono na sabuni katika shule za sendari Mgulasi, uwanja wa taifa na Bondwa pamoja na shule za msingi za Chamwino A,Chamwino B,Jitegemee na Kambarage katika kipindi cha covid 19,ugonjwa ambao licha ya kuwa nchi nyingi duniani wananchi wake wanaendelea kuugua lakini hapa nchini ugonjwa huo hakuna.

TIMU YA MAAFISA WA SHIRIKA LA KINARA WAKIWA KATIKA  HATUA YA AWALI YA KAMPENI DHIDI YA COVID 19,MANISPAA YA MOROGORO
“Hivi vifaa vya vya kukabiliana na corona tulivyovigawa katika shule vilisaidia kulinda wanafunzi wetu dhidi ya COVID 19 na kuwafanya wawe salama wakati wa masomo yao”Alisema na kuongeza, 

“Katika hata kipindi cha kufungua shule, tuliongeza juhudi kwa kuoongeza uelewa, kutoa mabango ya habari na kutoa ndoo za kunawa mikono, yote kusaidia kulinda wanafunzi dhidi ya COVID-19 katika shule  Mafiga Sekondari iliopo manispaa ya Morogoro, Walimu na wanafunzi wote walishukuru sana"

MIONGONI MWA SHUGHULI ZA SHIRIKA LA KINARA NI KUFUNDISHA USHONAJI WA NGUO KWA WASICHANA,SHUGHULI HIZO ZILIATHIRIKA NA JANGA LA COVID 19
Kinara mbali na kuendesha kampeni mbalimbali katika ngazi mbalimbali pia wanaendesha darasa la kujifunza ushonaji wa nguo lakini wakati wa covid 19 walilazimika kufunga darasa hilo kwa muda wa miezi miwili ambapo ili athiri kwa kiasi fulani mfumo wa kujifunza masomo hayo.

Aidha, alisema kwa sasa shule yake inaendelea na kuwapa ujuzi vijana kupata mafunzo ya jinsi ya kushona nguo mbalimbali ikiwemo sare za shule na mtindo mipya ya mavazi.

Kadhalika, katika kipindi cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika,Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya Kinara,Salu alisema kuwa walitumia fursa hicho kuwasisitiza wazazi na walezi kuwalinda watoto wao dhidi ya  covid 19.

Mhamasishaji jamii katika mabadiliko ya tabia (CCA) kutoka asasi ya Kinara Kassim Mahemu,kwa upande wake alisema walifika pia wananchi wa kata ya Sultan Area,Manispaa ya Morogoro kwa kutoa  elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya corona kwa kushirikiana na waafisa wa afya kutoka Manispaa ya Morogoro.

MAAFISA WA SHIRIKA LA KINARA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WAKATI WA KAMPENI DHIDI YA COVID 19
“Katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, kinara tulikuwa live kupitia Abood radio, kutoka shule ya sekondari Mgulasi waliongelea kuhusu siku ya mtoto wa Afrika wakilenga haki za watoto za kupata elimu hususani katika kipindi hiki cha COVID-19” Alisema Mahemu.

Leah Julius ni Afisa wa Kinara alisema kuwa katika kipindi cha covid 19 anakumbuka afanikiwa kuzungumza na  na wafanyabiashara wa soko la mjimpya,mjini Morogoro uelewa kwa wafanyabiashara ulikuwa ndogo jambo lililolezimika kutoa elimu ya kukabiliana na covid 19 kwa kuzingatia maelekezo ya serikali kupitia idara za afya kwa kunawa maji tiririka kwa  kuzingatia hatua sita kwa usahihi.

No comments:

Post a Comment