Loveness Nyawili
WAANDISHI wa habari mkoa wa Morogoro kupitia Klabu ya Waandishi wa habari (MOROPC) ameonesha hisia zao kwa uishukuru UTPC kwa kuajali waandishi wa habari kote nchini wakati wa covid 19.
Katika Mahojiano na Blog ya Moropc,baadhi ya wanachama wao akiwemo severin Blasio amesema kuwa UTPC imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia haki za waandishi wa habari ikiwemo kipindi cha corona ambap waandishi wa habari walipewa sabuni,vitakasa mikono na barakoa.
Aidha,Blasio amesema mbali na vitakasa mikono pia waandishi wa habari wamenufaika kwa kupewa mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na maambukizi mapya wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hususan kwenye mkusanyiko ya watu.
Mwanachama mwingine aliyenufaika na program ya UTPC katika kujali afya za waandishi wa habari ni Halfan Diyu ambaye amesema kuwa mazingira ya waandishi wa habari katika utendaji wa kazi unahitaji kuangaliwa na jicho la kipekee kwa kile alichokieleza ya kuwa mfumo wa utendaji wa kazi katika vyombo vya habari umebadilika.
“UTPC imekuwa ni dira na msimamizi mkubwa ya afya za waandishi wa habari kabla ya kipindi cha covid na baada ya kipindi cha covid UTPC imekuwa ikiwasimamia waandishi wa habari kupitia Klabu za waandishi wa habari zilizopo kila mkoa”Alisema Diyu.
Mwandishi mwingine aliyenufaika na msaada wa UTPC wakati wa COVID 19 ni Latifa Ganzel ambaye amesema waandishi wa habari wa kike nao wamenufaika na vifaa vilivyotolewa na UTPC ambao kwa Morogoro,uongozi wa Morogoro Press Club ulisimamia vema kwa kila mwanachama alinufaika kwa kupata vitakasa mikono(Sanitazer)
Alisema kuwa ni taasisi
chache za kihabari zilizopo hapa nchini ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika
kuangalia usalama wa waandishi wa habari wakati wa kazi,ambapo UTPC ni miongoni
mwao.
Nickson Mkilanya ni Mwenyekiti wa Morogoro Press Club kwa upande wake hakusita kuelezea mafanikio waliopata wanachama wake ikiwemo kuweka kumbukumbu sahihi wadau walionyesha utayari wao wakati wa covid ikiwemo serikali ofisi ya RAS ambao waliwapa uelewa waandishi wa habari juu ya historia ya covid 19 na nafasi ya waandishi wa habari katika kuchukua tahadhali wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Tanzania kwa sasa haina
ugonjwa wa corona ambapo wananchi wanaendelea kuchapa kazi,huku idara za afya
mjini morogoro ikiwahimiza wananchi kuzingatia kanuni za afya si kwa ajili ya
corona pekee bali pia kuepuka magonjwa ya mlipuko.
No comments:
Post a Comment