Breaking News

Dec 26, 2020

JANGA LA COVID 19 LIMEGHARIMU ZAIDI WANAWAKE DUNIANI

 

Wachuuzi wa mboga kwenye soko moja katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa (picha chanzo Habari UN)

JANGA  LA COVID 19 LIMEGHARIMU ZAIDI WANAWAKE DUNIANI

Peter Mgumia

WAKATI Watanzania wakiwa katika hali ya kumshukuru Mungu kwa kuepusha  wa janga la COVID-19 ambapo Tanzania imekuwa eneo salama dhidi ya corona,nchi nyingine duniani inaelezwa kuwa kuna  pengo la ukosefu wa usawa kati ya matajiri na maskini kuwa limeongezeka zaidi, halikadhalika umaskini, ikiwa ni mara ya kwanza katika miongo kadhaa.

 Kwa mujibu wa shirika la afya duniani zinaeleza kuwa janga COVID 19 limerudisha nyuma juhudi za kujenga zenye usawa zaidi Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, COVID-19 imeongeza pengo la ukosefu wa usawa, mtazamo ambao uliweka hadharani mwezi Februari mwaka huu  na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, likisema kuwa watu bilioni mbili wanaofanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi ndio walioathirika zaidi.

“Wanawake ndio wanagharimika zaidi katika janga la COVID-19 kwa kuwa wako katika nafasi kubwa zaidi ya kupoteza njia zao za kujipatia kipato na kuna nafasi finyu zaidi kwa wao kunufaika na mipango ya hifadhi ya jamii.”  Hiyo ni kauli ya Achim Steiner, Mkuu wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, akieleza madhara ya COVID-19 kwa wanawake, katika takwimu zilizotolewa mwezi Septemba.

Takwimu zilionesha kuwa viwango vya umaskini kwa wanawake viliongezeka kwa zaidi ya asilimia tisa, sawa na wanawake milioni 47, idadi inawakilisha kurejeshwa nyuma kwa mafanikio yaliyopatikana katika miongo kadhaa ya kutokomeza ufukara.

Phumzile Mlambo-Ngcuka, Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women, amesema ongezeko la wanawake wapo kwenye lindi la masikini kwenye mifumo inayounda jamii na uchumi.

Ingawa hivyo, Bwana Steiner amesisitiza kuwa mbinu zipo za kuboresha Maisha ya wanawake, hata wakati huu wa janga la sasa. Mathalani, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 100 wanaweza kuondolewa kwenye lindi la umaskini iwapo serikali zitaimarisha fursa ya elimu na uzazi wa mpango na kuhakikisha viwango vya mshahara ni vya haki na sawa na vile vya wanaume.chanzo Habari UN.

 

 

No comments:

Post a Comment