VICTOR MASANGU, KIBAMBA
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na vita
dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike na wakume
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development
(OCODE) limekuja na mpango wa kampeni maalumu ambayo itawasaidia
wanafunzi wa shule za awali na msingi zilizopo katika Manispaa ya
Ubungo lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo katika kupinga vitendo vya
ukatili.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo,
(OCODE),Joseph Jakson wakati wa sherehe za ufunguzi wa kampeni
maalumu ya siku 16 kwa ajili ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa
watoto wa kike zilizoandaliwa na shirika hilo kwa lengo la kuelimisha
jamii kuhusiana na vitendo vya ukatili ambayo imefanyika katika
kata ya kibamba manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Ocode Joseph Jakson katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ubungo ambapo waliweza kuhudhulia kwa lengo la kujionea mwenendo mzima wa program hiyo ambayo iliwajumuisha na wanafunzi mbali mbali.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa shirika hilo ambalo
lilianzishwa mnamo mwaka 1999 kwa sasa linatekeleza miradi mbali mbali ya
vijana lengo lake kubwa ikiwa ni kusaidia na kuiwezesha jamii kuweza kutambua
umuhimu wa elimu bora kuanzia ngazi ya awali pamoja na ile ya msingi kwa watoto
na kuwajengea vijana uwezo katika kuboresha masiha yao.
“Shirika letu la Ocode kwa kushirikiana na wadau pamoja na viongozi wa serikali kutoka manispaa ya Ubungo tumeona tumekuwa tukishirikiana bega kwa bega katika miradi yetu mbali mbali lakini kwa wakati huu tupo kwa ajili ya kuungana kwa pamoja kwa ajili ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo yanatarajia kufanyika kidunia Disemba 10 mwaka huu,”alisema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya ushauri wa masuala ya afya Dr. Cecilia Mkafu ambaye alikuwa mgeni rami katika halfa hiyo akizungumza jambo na wanafunzi wa shule za awali na msingi katika manispaa ya Ubungo ikiwa ni moja ya sherehe zilizofanyika kwa ajili ya kuelekea maadhimisho ya siku 16 ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia.Kadhalika, aliongeza kwamba wameamua kuzitumia siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuweza kutoa elimu mbali mbali
kwa vijana pamoja na wanafunzi kuhusiana na vitendo vya ukatili ili kuweza
kuona namna gani ya kuweza kuwapa fursa ya kujitambua na hatimaye kuendelea
kuishi kwa misingi ya kupatiwa haki bila uonevu wowote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya ushauri wa masuala ya afya Dr. Cecilia Mkafu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amebainisha kuwa katika kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike wanapaswa kuhakikisha wanajiamini na kujitambua pamoja na kupatiwa elimu ili waweze kutambua haki zao za msingi.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Ocode katika mwenye tisheti nyekundi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wanafunzi ambao waliweza kufanya vizuri katika mambo mbali mbali ikiwemo katika michezo ya mpira wa miguu.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
“Natambua kuna siku 16 za ukatili wa kijinsia ambazo uwa
zinaazimishwa kila mwaka kwa hivyo mimi kwa upande wake nalipongeza shirika la
Ocode kwa kuweza kutenga siku hii kwa ajili ya kufanya kampeni maalumu ambayo
imewashirikisha wanafunzi mbali mbali wa manispaa ya ubungo yote haya ni kwa
lengo la kushiriki na kujifunza mambo mbali mbali ya kupinga unyanyasaji wa
kijinsia.
Naye mmoja wa walimu waliohudhulia hafla hiyo, Amina
Muchumu amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanaondokana na wimbi la
kuwafanyia vitendo vya ukatili na unyanyasaji ya kijinsia watoto wao na badala
yake watilie mkazo zaidi katika kuwapeleka shule na kuimba serikali
kuwachukulia hatua kali kwa wale watakaobainika wanavunja sheria.
SHIRIKA la Organization for Community Development (OCODE)
ambalo limeanishwa mwaka 1999 limekuwa likishirikiana na serikali kwa hali na
mali katika kuisaidia jamii katika masuala ya kuleta maendeleo ikiwemo
kuwajengea uwezo vijana pamoja na wanafunzi wa shule za awali na msingi waweze
kujitambua katika mambo ya kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment