MWANDISHI WETU
Akizungumza na mwandishi wa
habari, meneja wa mwimbaji huyo, Paskal Linda maarufu Batarokota Nsumbantale
alisema
“ video na audio ya Nina
haja nawe imekamilika kwa asilimia mia na kuanzia Desemba 9, itakuwa kwa hewa,
hivyo mashabiki wa Maria Masao Kilasile wakae mkao wa kubarikiwa kwa nyimbo
hiyo”.
Aidha, Batarokota alisema kuwa mashabiki wa
injili waisubiri kazi na kuipokea kwa mikono miwili, kwamba nyimbo imetengenezwa
katika ubora wa kimataifa na studio ya
Sky Records iliyopo Kihonda, mjini Morogoro, chini ya prodyuza Orecy na
udhamini wa King David Foundation Co. Ltd
Maria Masao Kilasile ni mwimbaji
wa injili na mshirika wa kanisa la Winners linaongozwa na Askofu David Oyedepo,
hivyo Maria Masao Kilasile ataenda kutoa huduma katika kanisa lililo tayari kumwalika
popote na wakati wowote huyo tayari.
No comments:
Post a Comment