Askofu Mkuu Tanzania Assembly of God,Dk.Barnabas Mtokambali
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
ASKOFU Mkuu wa Kanisa
Tanzania Assembly of God (TAG), Askofu Barnabas Mtokambali ametoa siri jinsi viongozi
wenzake wa dini,wakiwemo maaskofu kutoka nje ya nchi walivyokuwa wakimpigia
simu mara kwa mara ili kujua iwapo Tanzania haina corona kama taarifa
zilivyoenea ulimwenguni
Askofu Mkuu Mtokambali,
alitoa siri hiyo kwa waumini wa kanisa la Gosheni lililopo Kilakala
mizambarani,Manispaa ya Morogoro,kwamba dunia imekuwa na gharika kubwa la
ugonjwa wa corona lakini Tanzania imekuwa tofauti kwamba gharika hilo
halikuwaathiri watanzania ulinganisha na mataifa mengine.
Amesema kuwa, Watanzania
wanapaswa kumshukuru Mungu kwa wema wake,kwa kutokuwa na athari kubwa dhidi ya corona kama ilivyo kwa
nchi nyingine,kwamba si watanzania ni wema sana bali ni mapenzi tu ya mungu kwa
watanzania.
“nilikuwa ninapokea simu
kutoka kwa maskofu wenzangu wakitaka niwafahamishe hali ya corona kwa Tanzania,lakini
ukweli ni kwamba Tanzania haina corona niliwahakikishia hivyo.”Alisema Askofu
Mtokambali.
Aidha,Askofu Mtokambali
aliendesha ibada maalum ya mshukuru Mungu kwa jinsi Mungu alivyoonesha maajabu
yake kwa watanzania ambapo licha ya kufanya mikusanyiko mbalimbali ikiwemo
kwenye ushiriki wa ibada lakini watu wamekuwa salama dhidi ya corona.
Amesema mataifa makubwa
duniani yanaendelea kuteseka dhidi ya corona hali hiyo imewasababishia wananchi
wa mataifa mengine wakiwa na hofu dhidi ya corona.
Hivi karibuni,serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Pombe Magufuli imeishangaza
ulimwengu kutokana na kitokomeza ugonjwa wa Covid-19 kwa kufanya maombi kwa
Mungu kila mmoja kwa imani yake,ambapo matokeo ya sala na dua zimeleta
mafanikio makubwa na taifa na linasonga mbele kiuchumi.
No comments:
Post a Comment