VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Mkoa wa Pwani,
Mhandisi Evarist Ndikilo, ameitaka jamii kuachana na tabia ya kuwabagua na
kuwanyanyapaa baadhi ya watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU),
badala yake wawape ushirikiano wa kutosha na kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali
za kuleta maendeleo pasipo kuwabagua.
Ndikilo, ametoa kauli hiyo,
wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambapo katika ngazi ya kimkoa
yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi majengo, Wilayani Bagamoyo, na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
pamoja na wadau mbalimbali wa afya kwa lengo la kuweza kutoa ujumbe walionao
kuhusiana virusi vya ukimwi (VVU).
“Kitu kikubwa mimi kama
kiongozi wetu wa Mkoa wa Pwani natambua kuwa mtu akipata maambukizi ya virusi
vya ukimwi sio kwamba ndio mwisho wake wa kufanya kazi au kuendelea kuishi,
kikubwa akizingatia vizuri maelekezo kutoka kwa watalaamu wa afya ataweza
kuishi kama watu wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ameshika na kuangalia moja ya bidhaa ambayo inazalishwa na kikundi cha wanawake wajasiriamali Wilayani Bagamoyo wakati wa sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya ukimwi duaniani amabyo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Bagamoyo.
kubwa zaidi ninawaomba
sana msiwanyanyapae kabisa kwani ni ndugu zetu na pia ni rafiki zetu tuendelee
kushirikiana nao katika mambo mbalimbali,”alisema Ndikilo
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi wote wa Halmashauri za Wilaya ya mji wa Kibaha, Mkuranga na Chalinze kuhakikisha kwamba wanaweka mpango mkakati kabambe ambao utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza hali ya maambukizi ya mapya ya Virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwani katika maeneo hayo hali sio nzuri kutoka na kuwepo kwa maambukizi kubwa.
Ndikilo alisema Halmashauri
hizo zimeeleza kuongoza kwa maambukizi mapya ya VVU huku chanzo kikielezwa kuwa
ni mwilingiliano wa shughuli za kiuchumi.
Alisema takwimu za maambukizi
kwa Mkoa huo za mwaka 2012 ni asilimia 5.9 na kwamba kimepungua
hadi kufikia asilimia 5.5 kwa mwaka 2017.
Alisema pamoja na kushukuka
kwa maambukizi lakini bado Halmashauri hizo zinaonekana kuwa na maambukizi
mengi sababu sikielezwa kuwa biashara, Viwanda vingi na vituo vya magari
makubwa.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo bada ya kupatiwa fursa ya kuzungumza na wananchi waliohudhuria katika sherehe hizo za siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani.
Hata hivyo, maambukizi kwa
wanawake kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu yanaelezwa kufikia
asilimia 4.3 huku wanaume wakiwa ni asilimia 3.6.
Ndikilo alisema moja ya
vikwazo vinavyoelezwa kuchochea maambukizi mapya ni pamoja na mila potofu, ndoa
za utotoni na ngoma za usiku.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa
Pwani D. Delphine Magere aliwataka wanawake wa mkoani humo kuwa wa
kwanza katika kukabiliana na wimbi la
maambukizi mapya ya VVU kutokana na umuhimu wao kwenye majukumu ya
kifamilia na kuhakikisha kuwa wanaendelea kujikinga zaidi ili wasiweze kupata
maambukizi mapya.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dr. Delphine Magere akifafanya jambo kwa wananchi na viongozi mbali mbali wa serikali na mashirika ya umma waakti wa sherehe za maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani amabyo kimkoa yamefanyika katika shule ya msingi majengo iliyopo Wilayani Bagamoyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa alisema kwamba katika kukabiliana na
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi wataendelea kushirikiana bega kwa bega na
wadau wengine wa sekta ya afya pamoja na kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi
juu ya umuhimu wa kuweza kwenda kupima ili kujua afya zao pamoja na kuzingatia
maelekezo mbali mbali ambayo yanatolewa na watalaamu wa afya.
Awali akisoma risala ya Watu
wanaoishi na VVU mmoja wa wawakilishi watu hao Elizabeth Hassan alisema kuwa
kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kikwazo
kilichopo katika kundi hilo ni baadhi ya Watu wanaoishi na VVU kusitisha
kutumia dawa za kurefusha maisha kitu ambacho ni kinyume kabisa na maelekezo
waliyoyopatiwa na madaktari.
Mmoja wa wawakilishi wa baadhi ya watu wanaoishi na maambukizi ya vurusi vya ukimwi VVU Elizabeth Hassan akisoma risala kwa mgeni rasmi kuhusiana na mwenendo mzima wa baadhi ya changamato mbali mbali wanazokutana nazo na kusaidiwa na serikali.
Mmoja wa kijana ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Bagamoyo,Juma Mohamed akiwa akitoa ushuhuda kwa mgeni rasmi kuhusu madhara yanayotokana na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo yalimsababishia kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi japo kwa sasa ameshaacha kutumia, kwamba anaendelea na matibabu.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment