Mhe Bahati Ndingo katikati akifuatilia kwa karibu taarifa ya Kituo cha Fungafunga kutoka kwa ofisa wa ustawi wa jamii, Mwamvita Kilima hayupo pichani wakati akiwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Fungafunga cha kuwahudumia wazee wasiojiweza Manispaa ya Morogoro.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro,Heri Hoza na kushoto kwake ni Katibu wa Mkoa Jumuiya hiyo,Mkoa wa Morogoro, Zuberi Mtelela(Picha na Severin Blasio)
Na Severin Blasio,Morogoro
MBUNGE viti maalum, kupitia Jumuiya ya wazazi ya Chama cha Mapinduzi, Bahati Ndingo amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli itaendelea kutatua changamoto zinazo wakabili wazee kwa ajili ya ustawi afya zao.
Mbunge Bahati akizungumza na Wazee wa Kituo cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya
Morogoro wakati wa ziara yake kituoni hapo alisema kuwa Wazee ni hazina hivyo
serikali kamwe haitawatupa kwa kuwa
wakati wa ujana wao walitoa mchango mkubwa katika kujenga taifa hivyo wanapaswa
kuhudumwia kikamilifu.
“Hawa
wazee ni baraka kuwa na sisi kama Jumuiya ya wazazi tutafikisha kero zenu
serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi na changamoto zile zilizopo kwenye uwezo
wetu tutaendelea kuzitatua”Alisema
Mhe.Bahati Ndingo akikabidhi sehemu ya msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu katika Kituo cha Wazee cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya Morogoro.
Katika ziara hiyo mdaku alitoa msaada wa
vyakula mbalimbali ikiwemo mchele mafuta ya kula sukari na sabuni.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Ofisa Mfawidhi wa kambi hiyo ofisa wa ustawi wa jamii,
Mwamvita Kilima alishukuru mbunge huyo kwa msaada alioutoa.
Kilima
aliwataka wadau wengine kuiga mfano huo na kwamba wakumbuke kuwa nao
ni kundi la wazee watarajiwa hivyo wanahitajika kutoa huduma za karibu mara kwa
mara ikiwa ni moja ya hatua ya kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.
Hata
hivyo, Kilima alitoa changamoto zinazoikabili kambi hiyo kuwa pamoja na
barabara ,uzio,bwalo la chakula na magodoro.
Akiongea
kwa niaba ya wazee wenzake, Mzee Joseph Kaniki alishukuru serikali
ya awanu ya tano kwa kuwajali wazee na kwamba wazee hao wanamwombe dua Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aweze kutekeleza majukumu yake vizuri akiwa na
afya njema.
No comments:
Post a Comment