WANAHABARI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA
WAANDISHI
wahabari wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kuepuka kuingia
kwenye migogoro wakati wa kuripoti habari kuelekea katika kipindi cha uchaguzi
mkuu Oktoba 2025.
Peter
Kimath,Elizabeth Tanzania na Peter Laurence ni wakufunzi waliojengewa uwezo na
UTPC kwa kushirikiana na IMS kwa lengo la kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
juu ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari sanjari na usalama mtandaoni
na masuala ya saikolojia ya maisha kwa waandishi wa habari.
Peter
Kimath amesema msingi bora wa mwandishi kufanya kazi zake vizuri bila kuingia
kwenye changamoto ni kufuata sheria zinazomuongoza,kufuata sheria za nchi na
kuangalia sera za chombo anachofanyia kazi kwa lengo la kulisha walaji wake
kile wanachotegemea
“tunapaswa kuelewa sheria na kanuni zinazohusu uchaguzi na vyombo vya habari, kama Sheria ya Huduma za Habari (2016), Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015) na Kanuni za Tume ya Uchaguzi.”anasema Kimath.
Halfan Diyu ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo akichangia madaMwandishi
Nguli,Halfan Diyu anasema mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani
yamewakumbusha vitu vingi muhimu vya kuzingatia wakati wa kuripori habari za
uchaguzi na nyingine katika jamii.
“tunaishukuru
UTPC na IMS kwa kuona umuhimu wa mafunzo
haya kwetu,naamini tutayatumia vizuri katika kuripoti habari,na kufuata maadili
ya kiuandishi ili kuepuka kuingia kwenye msigano.
Hamida
Shariff ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo anasema kutokana na
teknolojia vitu vinabadilika kila siku katika tasnia ya habari,hivyo wanahabari
wanapaswa kukumbushwa kila wakati katika masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi wa
taarifa binafsi na sheria zinawaongoza.
“nimejifunza
vitu vizuri vitakavyonisaidia katika utendaji wangu wa kazi kila siku
ikiwemo,namna ya kulinda vifaa vyangu vya kazi,kujilinda wakati wa kuripoti
habari uchunguzi,UTPC nawaomba kuendelea kutoa mafunzo kama haya kwani bado
wanahabari tunachangamoto nyingi zinahitaji kutatuliwa kwa njia ya kupewa
elimu".


No comments:
Post a Comment