WANAHABARI MOROGORO WAPEWA MAFUNZO KUFANYAKAZI KWA WELEDI
Baadhi ya washiriki na wanachama wa MoroPc wakifuatilia kwa umakini mafunzo yalioandaliwa na UTPC kwa kushirikana na IMS.Na Mwandishi wetu
WANAHABARI wametakiwa kuhakikisha
Wanafanya kazi kwa uhuru bila hofu ya kudhuriwa.Wanalindwa dhidi ya unyanyasaji
wa kimwili, kisaikolojia au kisheria.
Peter Laurence,Elizabeth
Tanzania na Peter Kimath ni wakufunzi waliojengewa uwezo na UTPC kwa
kushirikiana na IMS kwa lengo la kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya
ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari sanjari na usalama mtandaoni na
masuala ya saikolojia ya maisha kwa waandishi wa habari.
Laurence alisema waandishi
wa habari wanapaswa kuongeza umakini wanapotumia mitandao ya kijamii wakati
wanapotimiza wajibu wao,kwani kutawaweka salama na kuepuka kudukuliwa kazi zao.
Peter Kimath alisema kuwa
waandishi wa habari wanapaswa kupewa mazingira salama ya kufanya kazi, hasa
wakati wa kuripoti katika maeneo hatarishi (kama maandamano, migogoro ya
kisiasa, au vita).
Kimath akiwasilisha mada
kwa waandishi wa habari wa Morogoro kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa
habari alisema waandishi wa habari wazingatie weledi wanapotimiza wajibu
wapo,pia wanapokabiliwa na changamoto na kadhia katika mazingira ya kazi,ambayo
yanaviashiria hatarishi wawasiliane na viongozi wa Klabu za waandishi.
Mada ya saikolojia ya
maisha katika mazingira ya waandishi wa habari iliwasilishwa na Elizabeth
Tanzania ambaye aliwakumbusha waandishi wa habari kutambua jinsi athari ya Trauma
(Kiwewe) na namna ya kukabiliana nayo.
Aliwaeleza waandishi
wanapaswa kutambua maana ya trauma wa kuielezea kuwa ni hali ya maumivu makubwa
ya kihisia au kiakili yanayosababishwa na tukio la kushtua sana, kama kubakwa,
ajali mbaya, au kushuhudia vifo. Hali hii huweza kuathiri maisha ya mtu kwa muda
mrefu.
Elizabeth Tanzania,Mwezeshaji akiwa makini katika kuwasilisha mada kwa waandishi na wanachamawa Morogoro.“dalili ya trauma ni kumbukumbu
mbaya zinazojirudia (flashbacks), kujitenga na watu, hofu au mshangao kupita
kiasi,Kutojiamini, na kukosa usingizi”

No comments:
Post a Comment