RAIS SAMIA APONGEZWA UWEKEZAJI KWA WALIMU KATIKA TEHAMA
Na Thadei Hafigwa, Morogoro
WALIMU
zaidi 5000 wa shule za sekondari hapa nchini kutoka kanda 7 wamenufaika na
mafunzo ya TEHAMA katika kipindi cha miaka mitatu, ambapo kwa mwaka huu pekee,
walimu 1,870 wameshiriki mafunzo
hayo yaliyofanyika katika vituo vya Tukuyu
- Mbeya na Chuo cha Ualimu
Morogoro kutokana na uwekezaji uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Edward Wawa alibanisha hayo katika mjini Morogoro katika hafla ya kufunga mafunzo ya awamu ya tatu kwa walimu kutoka mikoa ya Morogoro,Pwani,Dar es Saalam,Lindi na Mtwara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Edward akiwasilisha taarifa yake kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dk.Hussein Omary.Wawa
alisema kuwa kuwa serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeanza
kutekeleza mradi wa kuboresha elimu ya sekondari kwa kuimarisha ujuzi wa walimu
kupitia mafunzo ya TEHAMA toka mwaka
2022 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kiashiria na 9 cha mradi wa matokeo
makubwa kinacholenga kuwajengea walimu uwezo wa kufundisha kwa kutumia mbinu za
kisasa na vifaa vya kidijitali.
Mafunzo
hayo yametekelezwa kwa awamu tatu,kwa kuzingatia kanda 7 zilizopo,katika awamu
ya kwanza,iliyofanyika mwaka 2022/2023,walimu 500 kutoka kanda ya kati na kanda
ya kaskazini,walipatiwa mafunzo hayo.
“Awamu ya pili yalifanyika mwaka 2023/2024 ambapo walimu 2632 kutoka kanda ya Ziwa,kanda ya magharibi,kanda ya kaskazini na kanda ya kati,walipatiwa mafunzo”alisema.
Baadhi ya Walimu Washiriki wa mafunzo ya Tehama mjini Morogoro walifuatilia kwa umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi,Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Hussein Omary (hayupo pichani) kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliofanyika katika Chuo cha Ualimu,Morogoro.Aidha,alifafanua
kuwa awamu ya tatu ya mafunzo kwa walimu wa Tehama yamefanyika katika mwaka 2024/2025
kwa kuhusisha vituo viwili,kituo cha kwanza Tukuyu Mbeya yalianza Julai 14-18,2025
na kuwanufaisha walimu 941,na Morogoroo ambapo jumla ya walimu 929 wamenufaika
na mafunzo hayo.
Mgeni
Rasmi wa hafla hiyo ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Hussein Omary, ambapo ametoa wito kwa walimu nchini kutumia
maarifa waliyopata katika mafunzo ya kitaaluma kuleta mabadiliko chanya katika
sekta ya elimu, akisisitiza kuwa elimu jumuishi na yenye usawa ni msingi wa
maendeleo endelevu ya taifa.
Dk.
Hussein alisema kuwa serikali ina dhamira ya dhati ya kuwekeza kwa walimu ili
kuimarisha elimu bora inayomfikia kila mtoto, bila kujali mahali alipo,wizara
yake inaendelea kutekeleza sera ya elimu kwa vitendo, kwa kuweka mkazo katika
mitaala, miundombinu, TEHAMA na maendeleo ya walimu ili kuhakikisha maono ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Sami Suluhu Hassan yanatimia.
“Mafunzo haya ni tafsiri ya maono ya Mheshimiwa
Rais. Tunatekeleza kwa vitendo sera ya elimu jumuishi na bora. Lengo ni
kuhakikisha kila mtoto anapata elimu sawa,bila kujali eneo analotoka,” alieleza.
Dk. Hussein alisisitiza nafasi ya walimu kama nguzo kuu ya mabadiliko katika mfumo wa elimu nchini, akisema mafanikio ya elimu hayawezi kupatikana bila uwekezaji wa kweli kwa walimu.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya kufunga mafunzo kwa walimu wa sekondari juu ya TEHAMA,Mjini Morogoro
Aidha,
alibainisha kuwa serikali imeanza kuimarisha miundombinu ya kufundishia kwa
kutumia TEHAMA ili kukabiliana na changamoto za karne ya 21, huku akiwataka
walimu kuwa mfano kwa jamii kwa kuonyesha weledi, maadili na ubunifu katika
kazi zao.
Mafunzo hayo yamewahusisha walimu kutoka shule mbalimbali nchini yakiwa na malengo kuwajengea uwezo kwa kutumia vifaa na rasilimali za Tehama darasani,kuongeza ubora wa utoaji wa elimu kupitia mbinu shirikishi za kidigitali,kuimarisha matokeo ya ufundishaji kwa wanafunzi kupitia teknolojia.




No comments:
Post a Comment