KUELEKEA mwishoni mwa mwezi Novemba mwimbaji wa muziki wa Injili Maria Masao Kilasile mwenye maskani yake Morogoro. Maria Masao Kilasile ambae ni Mshirika wa Kanisa la Winners kwa Askofu David O. Oyedepo mwezi huu wa Novemba ameanza maandalizi ya kurekodi video ya wimbo "Nina Haja Nawe".
Akizungumza na Blogu ya Moro Press Club Meneja wa Mwimbaji huyo, Paskal Linda maarufu Batarokota alisema ''wimbo Nina Haja Nawe maandalizi ya kurekodi video hiyo,yamekamilika kwa asilimia 100.
"Muda mfupi ujayo Maria Masao atakuwa location kwa ajili ya kuchukua picha za video chini ya watayarishaji kutoka kampuni ya studio za Sky Record ya Morogoro'' alisema Batarokota.
'Maria Masao Kilasole ni mwimbaji wa Kanisa la Winners Morogoro pia ni kiongozi katika uimbaji wa kusifu na kuabudu hivyo nawaomba mashabiki wa nyimbo za injili kumpa sapoti ili huduma yake izidi kukua na kuitangaza injili’, alisema Batarokota.
Maria
Masao Kilasile yuko chini ya lebo na udhamini wa kampuni ya
King David Foundation Co. Ltd iliyopo mjini Morogoro. chini ya Mkurugenzi John
Kilasile.
No comments:
Post a Comment