MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Silvestry Koka
NA MWANDISHI WETU
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la
Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Silvestry Koka
ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama
kwa wananchi wanaoishi katika Kata ya Pangani ili kuondokana na adha ya kutembea
umbali mrefu usiku na mchana kwa ajili ya kwenda kutafuta maji katika maeneo
mengine.
Koka aliyasema hayo
wakati akizungumza na baadhi ya wananachi kutoka mitaa mbali mbali ya Kata ya
Tanginini wakati wa mkutano wake maalumu wa kampeni wenye lengo la kunadi sera
zake pamoja na kuomba kura kwa wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika octoba 28 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi katika halmashauri ya Mji Kibaha Maulid Bundala akiwa anafafanua jambo katika mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya kuwanadi wagombea mbali mbali wa nafasi z a Urais, Ubunge pamoja na Udiwani.
Mgombea huyo aliongeza kuwa
lengo lake kubwa endapo wananchi watamchagua tena kuongoza katika kipindi cha
miaka mitano mingine kipaumbele chake kikubwa ni kuhakikisha anawaondolea
tatizo la ukosefu wa maji na kwamba kuna fedha ambazo zimeshatolewa na
serikali kwa ajili ya miradi mbali mbali katika maeneo mbali mbali.
“Natambua kuna baadhi ya
maeneo katika Kata ya Pangani kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi na
salama lakini katika kipindi kilichopita nilishapambana kuhakikisha kwamba
mradi wa maji unakuwepo kwa ajili ya kuweza kuwanufaisha wananchi wa mitaa
mbali mbali na kwamba leo nimeweza kupata fursa ya kutembelea matanki makubwa ambayo
yataweza kuwa na ujazo wa lita nyingi zzinazoweza kuondoa kabisa tatizo hili la
maji.
Aidha Koka alisema kwamba kuna
baadhi ya maeneo mengine katika kata ya Pangani yameshafaidia na huduma ya maji
safi na salama hivyo sehemu ambazo bado hazijasambaziwa maji lazima zitapata
maji kutokana na juhudi ambazo ameshazifanya katika kipindi kilichopita kwa
kushirikiana na serikali ili kuona wananachi wanaondokana na hali ya usumbufu
kila kukicha.
Akizungumzia suala la
miundombinu ya barabara Koka alifafanua kwamba nia na madhumuni yake ni
kuhakikisha anaboresha baarabara mabli mbali za mitaa ili ziweze kufanyiwa
ukarabati na hatimaye kuweza kupitika kwa urahisi katika kipindi chote hasa
katika kipindi cha mvua zinaponyesha kwani kumekuwepo na chanagmoto katika
baadhi ya miundombinu kuharibika.
Mgombea wa nafasi ya Udiwani wa katika Kata ya Pangani Augustino Mdachi (kulia) akiwa amesimama katika jukwaa moja na Mgomea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakati wa kuomba kura kwa wananchi wa kata ya Pangani.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa kata ya Pangani Augustino Mdachi alisema kwamba katika kata yake kwa kipind miaka ya nyumba kulikuwepo na chnagamoto mbali mbali lakini kutoka na juhudi amabzo alizifanya kwa kushirikiana na wananchi wake waliweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta mbali mbali za afya elimu pamoja hudumu nyingine za kijamii.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha
mapinduzi Halmashauri ya Wiaya ya Kibaha mji Maulid Bundala aliwawataka
wananchi kuhakikisha wanafanya maaamuzi ambayo ni sahihi kwa kuwachaguz
viongozi wa ccm ambao wanaweza kuwaletea mabadiliko ya kimaendeleo kutokana na
kutimiza yale yote ambayo yameandika katika utekelezaji wa ilani ya chama.
No comments:
Post a Comment