Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimboa la Kibaha Mjini Silvestry Koka.
Mgombea ubunge wa jimbo la
Kibaha mjini, Silvestry Koka kupitia tiketi ya Chama
Mgombea wa nafasi ya
Ubunge katika jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akiwa katika mkutano wake
wa kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi wa kata ya Mbwawa huku akiwa
sambamba kulia kwake na mgombea udiwani wa kata hiyo ya Mbwawa Judishi Mluge.
Koka alisema hayo wakati
akizungumza katika mikutano yake ya kampeni kwa wananchi wa Kata
mbili za Viziwa ziwa pamoja na wananchi wa Kata ya Mbwawa kwa ajili ya kuweza
kujinadi na kuomba kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Octoba 28 mwaka huu na kuahidi kuleta maendeleo katika nyanja tofauti na
kutatua changamoto zinazowakabili wananachi.
Alifafanua kwamba anatambua kuna baadhi ya maeneo yaliyopo katika kata ya viziwaziwa hawana huduma ya maji hivyo atahakikisha kwamba anaendelea kuongeza jitihada zaidi kwa kushirikiana bega kwa began a serikali katika kuwaondolea adha ya ukosefu wa maji wananchi hao ambao wamekuwa wakipata shida ya kutembea umbari mrefu.
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa anakata utepe
sambama na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi ngazi ya kata na Wilaya
ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa shina la wakereketwa wa ccm katika mtaa wa
segereni kata ya Viziwaziwa kabla ya kuanza kwa mkutano waake wa kampeni kwa
ajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na kujinadi ili kuomba kura.
“Ndugu zangu wananchi wa mtaa
wa Sagare katika kata hii ya Viziwaziwa natambua kuna changamoto ya upatikanaji
wa maji katika baadhi ya maeneo lakini mimi endapo mtanichagua na kunipa kura
nyingi katika uchagzui huu ambao unatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 28 mwezi
huu nitapambana vilivyo ili tumewe kumalizie mikakati ya kusambaza maji katika
kila nyumba kwa maana nilishapambana na baadhi ya maeneo wameshaaza kupata
huduma ya maji kwa hivyo kikubwa ni kunichagua kwa kishindo,”alisema Mgombea
huyo.
Mmoja wa viongozi wa wakinamama wa ccm katika shina hilo akisalimiana na mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kibaha mji Silvesty Koka wakati wa sherehe za uzinduzi wa shina hilo namba moja la wakereketwa wa kata ya viziwaziwa.
Kadhalika alisema kwamba pamoja na kupambana na katika huduma ya maji pia ameahidi kulivalia njuga ssuala la kuanzisha mradi wa ujenzi wa shule ya msingi kwa lengo la kuweza kuwaondolea adha kubwa watoto wadogo kutembea umbari mrefu kwenda katika maeneo mengine na kwamba suala hilo anashukuru kwa kuwa serikali ya mtaa imeshapata eneo kwa ajili ya ujenzi huo.
Koka pia aliwaeleza wananchi
wa kata hiyo ya Viziwaziwa kuweka mipango madhubuti katika suala zima la
upatikanaji wa huduma ya afya ikiwemo sambamba na ukarabati wa
miundombinu ya barabara za mitaa ili ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi
chote hasa katika nyakati ya mvua zinaponyesha wananchi wasipate shida ya
kuvuka katika baadhi ya maeneo.
Katika hatua nyingine Mgombea
huyo wa Jimbo la Kibaha mjini akiwa katika mkutano wake wa kampeni kwa wananchi
wa kata ya Mbwawa aliwaeleza nia yake na dhamira katika kuwaondolea changamoto
mbali mbali zinazowakabili iliwemo ukosefu wa nishati ya umeme, huduma ya
upatikanaji wa maji pamoja na ukosefu wa usafiri wa uhakika.
“Ndugu zangu wananchi wa kata
hii ya Mbwawa nataka kuwahakikishia kwamba mimi kama mgombea wenu wa jimbo hilo
la kibaha mjini nipo pamoja na nyinyi katika suala zima la kuleta maendeleoa na
mbwawa ya wakati ule sio ya sasa kwani kila kukicha chachu ya maendeleo
inaonekana hivyo pindi mtakaponichaguza tena yale mambo yote mazuri ambayo
tumeshaanza kuyatelekeza ni lazima tusimame imara katika kuyaendelea kwa nguvu
moja,”alisema Koka.
Kwa upande wake mgombea kiti
cha Udiwani katika kata ya Mbwawa Judith Mruge alisema kwamba kiti
kikubwa kilichomsukuma kuwania katika nafasi hiyo ni kushirikiana na wananchi
pamoja na serikali kwa lengo la kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo
kusikiliza kero zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Naye Mgombea Ubunge kupitia
viti maalumu Mkoa wa Pwani kwa tiketi ya CCM Hawa mchafu alisema kwamba
wananchi ni lazima wahakikishe wanaunga mkono juhudi ambazo zimefanywa na Rais
wa awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli na kuhakisha kwamba wanachagua viongozi
ambao ni wazalendo na nchi yao ili kuweza kuwaletea maendeleo na kuachana na
wengine ambao wanaweza kuleta uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment