Breaking News

Nov 26, 2020

DIWANI MANISPAA MOROGORO ASAIDIA CHAKULA WATAHINIWA DARASA LA NNE


 Diwani wa Kata ya Tungi,Manispaa ya Morogoro, Nimala Mchunguzi (kulia)akimkabidhi Msaada  wa Tsh 630,000  kwa Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Tungi Rehema Namkunda kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne walioanza mtihani yao Novemba 25.

Na Severin Blasio, Morogoro

 DIWANI mteule wa kata ya Tungi manispaa ya Morogoro Namala Mchunguzi ametoa msaada wa shilingi 630,000/=pamoja na kilo 80 za mchele kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya msingi Tungi wanalianza kufanya mtihani Novemba 25 mwaka huu.

Msaada huo umetolewa ikiwa ni kuwajengea wanafunzi wa darasa la nne kuwa na ari ya  kufanya mtihani ili wafanikiwe kufaulu kuelekea darasa la tano.

Akitoa msaada huo Mchunguzi alisema ametoa msaada huo ili wanafunzi hao waweze kufanya mtihani huo kwa kujiamini huku wakipata chakula shuleni kwa ajili ya kufanya vizuri.

“Nimeleta msada huu uwasaidie wanafunzi watakaofanya mtihani darasa nne kufauru mtihani unatakiwa ufanye ukiwa umeshiba,lakini ukiwa na njaa huwezi kufanya vizuri"alisema Mchunguzi.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Rehema Namkunda amepongeza Diwani huyo kwa msaada huo ambapo aliwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia mambo mbalimbali ya elimu.


Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Tungi Rehema Namkunda baada ya kukabidhiwa msaada wa mchele kilo 80 kutoka kwa Diwani wa Kata ya Tungi,Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne walionza mtihani yao Novemba 25.

Jumla ya wanafunzi 150 kwenye shule ya msingi Tungi,Manispaa ya Morogoro wamefanya mtihani wa darasa la nne.

Shule ya msingi ya Tungi yenye idadi ya wanafunzi zaidi ya 1400 inakabiliwa na changamoto lukuki moja ikiwa ni wanafunzi wake kutopata chakula cha mchana uhaba wa miundombinu ya madarasa,vyoo na samani

 

No comments:

Post a Comment