Breaking News

Dec 3, 2025

TAWA WAPEWA MKAKATI USALAMA WA BINADAMU NA WANYAMAPORI

 WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,DKT.ASHATU KIJAJI(MB) 

MAKALA MAALUM

 ZIARA YA   KIMKAKATI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MKOA WA MOROGORO

Na Thadei Hafigwa

 ILIKUWA ni ziara ya kimkakati  aliyoifanya  WAZIRI wa maliasili na Utalii,Dkt.Ashatu Kijaji(MB) ambapo ilitoa mwelekeo na maelekezo kwa mamlaka ya wasimamizi wa wanyamapori Tanzania(TAWA) kwa kutaja vipaumbele kwa kuzingatia  maagizo ya Rais wa Jamhuri Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan yaweze kutekelezwa kwa vitendo kwa masilahi ya nchi.

Waziri Kijaji amebainisha hayo mijini Novemba 24 Morogoro akiwa katika ziara yake ya kwanza toka ateuliwe kushika wadhifa huo katika kipindi cha pili cha awamu ya sita ya Rais Samia na kuongea na menejimenti ya TAWA,sanjari na kushiriki kwenye hafla ya kuzindua vitendea kazi kwa menejimenti na watumishi wa taasisi ya TAWA ambavyo ni magari 4,Pilipiki 33 na ndegenyuki ikiwa ni mkakati wa kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wao.

Dkt.Kijaji alirejea hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 aliyoelekeza wizara ya maliasili na utalii na tasisi zake kuhakikisha wanaendelea kuimarisha ulinzi wa maeneo ya hifadhi na udhibiti wa wanyamapori na waharibifu dhidi ya mali na maisha ya wananchi.

Alisema kuwa,tayari serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan imeshaelekeza na kutoa nafasi ya kuajili watumishi na askari wa wanyamapori ili kwenda kuwahudumia wananchi na kupunguza kero dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo yao.

”tunatakiwa tuendelee na ujenzi wa vituo vya ulinzi,tunatakiwa kuwa na mbinu za kisasa zaidi,na vifaa pia vya kisasa ikiwemo ndegenyuki,ambavyo tumezindua,tumizindua  magari,tumezindua pikipiki kwa hiyo hatuna visingizio tena kushindwa kuwahumia twendeni tukawadumie wananchi wetu”alisema.

“hivyo tunatakiwa kwenda kufanyakazi ya huduma kwa wananchi wetu  kwa kujali utu wao”

Waziri aliitaka menejimenti ya TAWA kujipanga katika kuhakikisha ya kuwa wanakwenda kutekeleza maelekezo hayo kwa weledi ili watanzania kuendelea kunufaika na rasilimali zao walizojaliwa na Mwenyezi mungu.

Aliwakumbusha kutambua kuwa msingi wa uwepo wa taasisi ya tawa ni  ulinzi wa wanyamapori bila ya kuwepo kwa jambo hilo hakutakuwemo kwa taasisi hiyo,hivyo wanapaswa  kuongeza ufanisi wa doria,itelejensia na matumizi ya teknolojia,ndegenyuki,kisukuma mawimbi,na vifaa rafiki vya ulinzi ili kulinda rasilimali muhimu zilizopo hapa nchini.

Aidha,mkakati mwingine alitaja ni kuzuia kwa kiwango cha juu vitendo vya ujangili ,uharibifu wa mazingira na biashara haramu za nyara ya serikali.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt Ashatu Kijaji(katikati) akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa vitendea kazi kwa maafisa wa wanyamapori mjini Morogoro alipofanya ziara ya kikazi,wengine walishiriki kushika utepe kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ta wanyamapori Tanzania(TAWA),Meja Jenerali Mstaafu,Hamis Semfuko,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Hamad Chande,kutoka kushoto kwa Mhe.Waziri Kijaji ni Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA),Mlange Kabange

Pia,alihimiza kuendelea ushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha maeneo yote chini ya tawa yanabaki salama na hakina anayeyachezea.

Suala lingine aliloliwekea kipaumbele ni kuhusisha mifumo ya taarifa,uchaguzi na tathmini ya matukio ili maamuzi ya kiutendaji yawe haraka,sahihi na yakiufanisi zaidi.

Alisisitiza na kuagiza kwamba hawatavumilia upotevu wa rasilimali za taifa,kwa kuwa Tawa wamewezeshwa kwa rasilimali  zote na utayari wa serikali ya awamu ya sita ni mkubwa katika kuhakikisha inaendelea kuweka mazingira  wezeshi ili kurahisha kutendaji kazi kwa urahisi zaidi.

Aidha,Waziri huyo wa maliasilia na utalii aliwataka tawa kuimarisha mapato na uendelevu wa taasisi kwa kujenga uwezo wa kifedha utakawezesha kulinda na kuendeleza maeneo yote walioaminiwa na kukabidhiwa na watanzania.

Alitoa maelekezo ya kuendelea kumaisha ukusanyaji wa mapato,kuhakikisha hakuna uvujaji na kuongeza ufanisi wa mifumo ya kifedha,ni muhimu sana mifumo ikasomana.

Aliweka mkazo kwa menejimenti ya tawa wa matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa mapato ndani ya taasisi na kamwe kutoruhusu ukusanyaji wa fedha zikiwa mbichi,na kutumika zikiwa mbichi ili kuleta ufanisi na kurahisa kufanya tathimini kilichokusanya na kutumika katika mwaka uliopita.

Kadhalika aliwataka kuboresha fursa za uwekezaji rafiki hususan zenye tija katika mazingira yanayowazunguka katika maeneo ya utalii wa ekolojia kwa kuweka kambi za kitalii,utalii wa picha kwa kuonesha uwezo katika utendaji kazi.

Alihimiza menejimenti ya tawa kuongeza juhudi ya utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yote ya Tawa ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje,kwa ubunifu mbinu gani zitakazotumika katika kufanikisha jukumu hilo na kuibua vivutio vingine ili kufikia idadi ya watalii mil.8 kama ilivyoelekezwa katika ilani ya ccm 2025-2030.

“ni wazi tukafahamu bila ya  mapato hakuna maendeleo uendelevu wa taasisi yetu wala ya taifa letu,moja ya taasisi zinazotakiwa kuongeza mapato ni pamoja na taasisi yetu(tawa)”alisema

Alisema kila mmoja  alimsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia kwamba kipindi hiki ni cha kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini,kutumia mapato ya ndani ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo nchini.

Suala lingine alilosisitiza ni utoaji wa huduma kwa wananchi ni lazima ziweze kuzingatia utu,kwamba dhamira ya serikali ni kuwatumia watu kwa utu,heshima na haki,hivyo migongano katika ya watu na wanyamapori ishughulikiwe kwa haraka kwa kutumia uadilifu,weledi na vifaa na miundombinu ilivyopo katika kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao.

Alikemea tabia walionayo baadhi ya watumishi wa tawa ya kuwataka wananchi kuchangia gharama za mafuta.

“ipo tabia ya kuwaambia wananchi,kama unataka nije changia mafuta,jambo hilo halipo na katibu mkuu hili naomba ulisimamie ,mwananchi hatakiwi kuchangia mafuta ili askari wetu akifikie mwananchi,ipo tabia kwa baadhi ya maeneo.”alisema

Awali,Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA),Mlange Kabange,asema wapo tayari kuteleza maagizo yote yanayotolewa na serikali katika kuhakikisha malengo ya kuwahudumia wananchi yanafikiwa kikamilifu katika uhifadhi wa wanyamapori.

Kabange anasema kuwa tawa inajukumu la kusimamia mapori ya nje ya Tanapa na  Ngorongoro,wanasimamia mapori ya akiba 28,na mapori tengevu 23,yote kwa pamoja yana ukubwa wa kilometa za mraba 133,276.36,eneo hilo ni kubwa zinazidi ukubwa wa baadhi ya nchi.

Alisema kuwa tawa wanatambua kuwa wana jukumu la kuhakikisha rasilimali za wanyamapori  zinalindwa na kwamba wafanikio wanayopata yanatokana na serikali ya awali ya sita imekuwa ikiwapatia fedha za kuteleza bajeti zao kwa asilimia 100 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Alisema mbali ya fedha za bajeti,Rais Samia aliwapatia fedha za kuboresha miundombinu za utalii,katika kipindi cha oviko sekta nyingi zilitetereka, lakini tawa walipewa fedha bil 12.9 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii.

Sanjari na hayo,alisema kuwa maafisa na watumishi wa tawa waliongezewa mshahara na watumishi 3000 wenye sifa walipandishwa vyeo jambo ambalo ni rekodi ambayo haijawahi kutokea toka kuasisiwa kwa tawa.

Aliishukuru serikali kupitia Rais Samia kuwa sekta ya utalii imekuwa kutokana na filamu ya royal tour na kupelekea mwaka jana (2024) walipata kampuni ya uwekezaji kutoka china katika sekta ya utalii,jambo ambalo siku za nyuma halijawahi kutokea.

Aidha,alishukuru wizara ya maliasili na utalii kwa kuandaa miongozo,sera na kanuni zinazowarahishia taasisi kutekeleza majukumu yake sekta ya utalii wa uwindaji na utalii wa picha.

Naye,Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ta wanyamapori Tanzania(TAWA),Meja Jenerali Mstaafu,Hamis Semfuko alimpongeza Rais Samia kwa kupata ridhaa ya kuongeza taifa la Tanzania kwa kipindi cha pili cha awali ya sita,ambapo inatokana na imani waliokuwa nayo wananchi kwake na uchapakazi wake katika sekta mbalimbali.

Meja Jenerali Mstaafu Semfuko pia alionesha shukrani zake kwa serikali kwa kuweka mazingira wezeshi katika utekelezaji wa majukumu ya tawa katika ulinzi na uhifadhi wa wanyamapori na mazingira yake.

 Kwa upande wake Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt.Hassan Abbas alisema ziara waliifanya ni kutembelea jeshi la uhifadhi kujua kazi zinafanyika,mafanikio na changamoto zilizopo kwa wananchi wanaishi karibu na maeneo ya hifadhi na namna ya kukabiliana nazo.

Dkt. Abbas ametaja Tanzania inaongoza kuwa na simba wengi duniani wapatao 17,000,jumla ya chui 24,000 ambapo Tanzania inaongoza Afrika na duniani,huku idadi ya ni nyati 200,025,na tembo 60,000.

No comments:

Post a Comment