Morogoro Yaongeza Kasi ya kuvutia Wawekezaji yaweka mpango Mahususi
Na Mwandishi wetu
KATIKA kuhakikisha ya kuwa fursa za uwekezaji zinaeleweka kwa wanda mpana Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amewataka wataalamu na Taasisi zilizopo Mkoa wa Morogoro kuzielewa na kuzitambua fursa hizo ili ziweze kutangazwa na kufahamika kwa wawekezaji, wanachi na wadau wa maendeleo.
Akifungua kikao cha uhuishaji wa Muongozo wa fursa za uwezekezaji,Dkt Mussa amebainisha kwamba ili mpango huo uweze kutambulika na kueleweka wataalamu wa Mkoa huo wanapaswa kufahamu fursa za uwekezaji zilizopo katika njanya mbali mbali ikiwmo kilimo,utalii biashara na ufugaji pamoja na fursa za usafirishaji zilizopo ikwemo reli ya mwendo kasi (SGR).
"Morogoro tuna fursa nyingi tumezieleza? " amesema Dkt. Mussa.
Dkt Mussa ametoa wito huo,Julai 15,mwaka huu, ametaka utekelezaji wa mpango huo kushirikisha wanachi sio tu kufahamu fursa zilizopo pia kuwa sehemu ya utekelezaji wa mpango huo ili uwe na manufaa kwa jamii husika.
Aidha,Alisema kuwa mkoa wa Morogoro umejaliwa kuwa na rasilimali na fursa nyingi ambazo bado hazijatangazwa kwa kiwango kinachostahili.
Kwa upande wake, Mkuu wa sehemu ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mkoa wa Morogoro Bi. Beatrice Njawa amesema kuwa muongozo uliopo umepitwa na wakati hivyo unahitajika kuhuishwa na kujengewa uwelewa kwa Taasisi na Sekretariet ya Mkoa ili uweze kueleweka na hatimaye kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwa jamii.
Naye, Dkt Hoseana Lunogelo ambaye ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na kijamii Tanzania ( ESRF), amesema kuwa wao kama Taasisi wanashughulikia masuala ya utafiti kwa upande wa Serikali na Sekta binafsi hivyo Mikoa yote inahitajika kuandaa na kuanisha fursa za vivutio vya uwekezaji vilipo kwenye maeneo yao ukiwemo Mkoa wa Morogoro.
Dkt Lunogelo amesema kuwa



No comments:
Post a Comment