JUMUIYA YA WAZAZI UWANJA WA TAIFA WAPONGEZA,RAIS SAMIA,MBUNGE NA DIWANI MATESA
Na Thadei Hafigwa
MSEMO wa Wahenga Chanda Chema huvishwa pete,umekuwa msemo maarufu katika matukio na hafla mbalimbali katika jamii kutambua mchango wa watu walitoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha malengo yaliokusudiwa.
Jumuiya ya Wazazi Kata ya Uwanja wa Taifa,Manispaa ya Morogoro wametumia kwa vitendo msemo huo kwa kuandaa hafla ya kupongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa,na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini,Abdulaziz Abood na Diwani wa Kata hiyo,Rashid Matesa kwa kuaminiwa na wananchi kwa kuchaguliwa katika nafasi zao katika uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana,2025.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa CCM kata ya Uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na wanachama na wapenzi wa chama hicho,huku msisitizo ukiweka,kuendelea kudumisha amani,upendo na mshikamano miongoni mwa wanachama,bila ya kujali itikadi na hali zao za kiuchumi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi,Kata ya Uwanja wa Taifa,Adili Omar aliwaasa wanachama kwamba shughuli za kisiasa isiwe uhasama,bali ni sehemu ya mchakato wa kupata viongozi bora,kwamba uchaguzi unapokwisha kila mmoja anapaswa kuzika tofauti zao wakati wa kampeni na kuimarisha umoja na mshikamano.
Omar alisema kuwa kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya wanachama pindi wanapogombea nafasi za uongozi,na inapotokea kura hazikutocha wanaendeleza chuki na uhasama na visasi jambo ambalo halina afya katika maisha ya wanasiasa.
"ninapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuongoza taifa letu amekuwa mstahamirivu,mchakapakazi na mwenye kujali shida za watanzania.Katika kata tumeletewa fedha za ujenzi wa wadi ya mama na mtoto katika zahahati yetu."alisema
Pia,alimpogeza Mbunge wa Morogoro Mjini,Abdulaziz Abood katika mchango wake katika kusimamia maendeleo ya wananchi,kwamba daima amekuwa mnyenyekevu na usiye na makuu katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananachi."Mbunge amekuwa na uso wa ukarimu kwa wananchi,welcome face"alisema.
Aidha,katika hafla hiyo iliyotanguliwa na kikao cha baraza la Jumuiya ya Wazazi baadhi ya viongozi walitunukiwa vyeti vya pongezi katika kufanikisha uchanguzi kuu wa mwezi Oktoba 2025,viongozi waliopewa tuzo ni kutoka jumuiya ya wazazi,Diwani wa Kata ya uwanja wa taifa,umoja wa wanawake (UWT),katibu Kata,na mwenyekiti waCCCM kata ya Uwanja wa taifa.
Kwa upande wake,Mwenyekti wa CCM kata ya Uwanja wa Taifa,Athman Mswagala aliwapongeza uongozi wa jumuiya hiyo kwa kuwa mafano wa kuigwa na jumuiya nyingin,kwa kile alichokieleza kwamba toka uchaguzi mkuu ulipokwisha hakuna jumuiya yoyote iliyowahi kufanya hafla kama ilivyofanywa na jumuiya ya wazazi.
Mswagala alisisitiza kuendelea kufanya shughuli za chama kwa kuzingatia katiba,kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza manung'uniko yakiyokuwa ya lazima,kwamba kila mwanachama akitimiza wajibu wake ustawi wa chama hicho utaendelea kushamiri na kuendelea kuaminika na kushika dola.




No comments:
Post a Comment