UONGOZI WA MOROPC WAWEKA MKAKATI WA 2026/2030, WATEUA LUCAS KUWA MWAKILISHI WA NANE NANE 2026
Na Thadei Hafigwa
UONGOZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (MOROPC) umepanga mkakati madhubuti wa kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali, lengo likiwa ni kuibua na kutekeleza miradi itakayosaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa chama kwa kipindi cha 2026/2030.
Mkakati huo ulijadiliwa katika
kikao cha Kamati Tendaji ya chama, kilichoongozwa na Mwenyekiti wake, Nickson
Mkilanya. Katika kikao hicho, Mkilanya aliwahimiza viongozi na wanachama wote
kutimiza majukumu
Mkilanya alieleza kuwa anaamini
MOROPC ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja waandishi wa habari wote katika mkoa
wa Morogoro, wakiwemo wale kutoka wilaya zote za mkoa huo. Alibainisha kuwa
katika mwaka 2025, waandishi wa habari kupitia chama hicho wameweza kutekeleza
wajibu wao ipasavyo katika matukio mbalimbali, ikiwemo maonesho ya wakulima
Nane Nane yaliyowashirikisha mikoa ya Pwani,
Akizungumzia mwaka 2026, Mwenyekiti huyo alisisitiza haja ya kuwa ubunifu zaidi katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Mashariki. “Tunapaswa kutimiza wajibu wetu kikamilifu. Katika maonesho ya Nane Nane, lazima twende kiubunifu zaidi kwa kutumia tathmini ya mwaka jana ili kuboresha utendaji wetu. Malengo yetu ni kuhakikisha kwamba dhana yetu ya ‘kuwa sauti kwa wasio na sauti’ inatekelezwa kivitendo,” alisema Mkilanya.
Katika hatua nyingine, wajumbe wa Kamati Tendaji wamemteua Katibu Mtendaji wa chama, Lilian Lucas, kuwa mwakilishi wa waandishi wa habari katika kamati ya habari, uhamasishaji na matangazo inayoshughulikia maandalizi ya maonesho ya Nane Nane kanda ya Mashariki. Uteuzi huu umetokana na utendakazi wake bora mwaka 2025.
Akikubali uteuzi huo, Lilian Lucas, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Morogoro Press Club, alieleza shukrani zake kwa wajumbe wa Kamati Tendaji chini ya uongozi wa Nickson Mkilanya kwa kuendelea kumuamini katika nafasi hiyo ya uwakilishi.
Lucas ameahidi kufanya kazi kwa weledi na bila ubaguzi wowote, akihakikisha kwamba kila mwandishi wa habari kupitia vyombo vyao mbalimbali anapata fursa ya kushiriki na kutekeleza wajibu wake ipasavyo. Amesema atajitahidi kuripoti matukio kwa usahihi na kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa maonesho ya Nane Nane kanda ya Mashariki.

No comments:
Post a Comment