WANANCHI WASHAURIWA KUEPUKA MATUMIZI YA DAWA KIHOLELA
Na Severin Blasio,Morogoro
WANANCHI
wameshauriwa kuacha tabia ya kununua dawa na kutumia bila ushauri wa daktari na
badala yake waende
kwenye kituo cha kutoa huduma wapate
ushauri wa kitaalam.
Kauli
hiyo imetolewa na mganga mfawidhi wa wa kituo cha huduma ya mama,baba na mtoto
cha Susannah Wesley (Polyclinic) Dkt Bahati Faustine kwenye uzinduzi wa jengo
la huduma ya mama,baba na mtoto.
Kituo
hicho kinamilikiwa na kanisa la The United Methodist Tanzania kilichopo kata
ya Kihonda Maghorofani kilikuwa kinatoa huduma ya wagonjwa wa nje (OPD) na kimeongeza jengo la mama,baba na
mtoto (RCH).
“Kumekuwa na tabia iliyojengeka miongoni mwetu ya mtu
anapojisikia kuumwa kwenda kwe nye duka la la dawa au tiba mbadalana kununua
dawa kisha kuzitumia bila
kujua anatibu nini.
“Na
wengine huenda mbali zaidi na kuwapigia simu baadhi ya watoa huduma wa za afya na kuuliza aina ya dawa ya
kumeza ili wapone jambo ambalo ni kinyume na kanuni za matibabu “Alisema Dkt
Faustine.
Dkt
Faustine alisema utaratibu wa matibabu unawataka
wananchi wanapojisikia wanaumwa kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha huduma
ili waonane na daktari ambaye atamsikiliza ,kumchunguza ,kumpima na baada ya
kugundua ugonjwa atamwandikia dawa za kutumia.
Aidha
Dkt Faustine ametoa shime kwa wazazi kujenga mazoea ya kuonana na wataalamu wa
masuala ya uzazi kabla ya hawajapata ujauzito sambamba na kuhimiza umuhimu wa mama na
mtoto kutumiza chanjo zote.
Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro,Hirary Sagara watatu kutoka kulia aliyevaa miwani akikata utepe kuashiria kuzinduzi wa Jengo la huduma ya afya kwa Mama,Baba na Mtoto(RCH) cha Sussanah Welsey Polyclinic iliopo Kata ya Kihonda Maghorofani,Manispaa ya Morogoro.
Alitoa
changamoto ya kituo hicho kuwa ni kutopata kibali cha huduma ya mfuko wa bima
ya afya,miundombinu ya barabara na ukosekanaji wa usafiri wa wagonjwa
wanaohitaji rufaa.
Akijibu
changamoto za kituo hicho,Mratibu wa huduma za afya Maispaa ya Morogoro Dkt
Felister Stanslaus kwa niaba ya mganga mkuu alimuhakikishia daktari wa kituo cha Susannah
wesley polyclinic kuwa serikali haitawaaacha nyuma wapo tayari kushirikiana nao
katika kuongeza ufanisi katika kutoa huduma hiyo.
Naye mgeni rasmi katibu Tawala Mkuu wa wilaya ya Morogoro Hilary Sagara alipongeza Kanisa la The uniteed Methedist kwa kuweza kusaidiana na serikali katika kupanua huduma za afya.
No comments:
Post a Comment