Ugonjwa
wa ‘Kimyanga’ wawasababisha hasara Wakulima wa mpunga Utengule
Na Thadei Hafigwa
WANANCHI wa
Kata ya Utengule,Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba katika msimu wa kilimo 2022/2023
wamekabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa zao la mpunga maarufu ‘Kimyanga’ ambapo wadudu waharibifu
wanashambulia kwa kuzorotesha ustawi wa zao hilo linapokuwa shambani.
Diwani wa Kata ya Utengule Ditram
Mhenga.alisema kuwa Ugonjwa wa ‘Kimyanga’ umepewa jina hilo na wenyeji kutokana
na jinsi mimea inavyonyauka ikiwa shambani umewasababisha wananchi wengi kupata
hasara kwa kuwa zao la mpunga linategemewa kwa chakula na biashara.
”Wananchi wangu ni wachapa
kazi sana,katika msimu huu wa kilimo,mazao yao yameshambuliwa na ugonjwa ambao
wataalamu wa kilimo wanaufanyia utafiti ili msimu ujayo wa kilimo ugonjwa huo
uweze kudhibitiwa katika msimu huu umewasumbua hata wataalamu wetu wa kilimo”.alisema.
Aidha,kuhusu upatikanaji wa
pembejeo katika msimu wa kilimo uliopita
alisema pamoja na jitihada zilizofanywa
na serikali katika kuhakikisha pembejeo za ruzuku zinawafikiwa wananchi lakini
wakulima wa utengule hawakunufaika kwa sababu kituo cha kuchukulia pembejeo
kilikuwa mbali.
Mzee Francis kinyanyilo (62)
ni mkazi wa Utengule alisema kuwa shughuli kuu wanazofanya ni kilimo cha mazao
ya Mahindi,Mpunga,Viazi lakini msimu wa mwaka huu shughuli zao ziliingia na dosari ya ugonjwa wa
Kimnyaanga ambao unakausha mazao.
“Binafsi nilipoona dalili
kwenye shamba langu lilikimbilia ofisi ya kata nilikutanna afisa kilimo alipatia
dawa ya kukabiliana na ugonjwa huo kwa kiasi fulani ilinisaidia,ila changamoto
ilikuwa ni kubwa sana kwenye upatikaji wa pembejeo.”alisema.
Mkulima mwingine aliyejitambulisha
kwa jina moja la Ramadhan alisema yeye katika msimu wa kilimo kwa mwaka huu
aliandaa shamba lake lenye ukubwa wa hekari saba ambalo alipanda zao la mpanga kutokana
na ugonjwa wa kimyanga amejikuta akipata hasara kubwa kwa kukosa mazao
shambani.
Hata hivyo,Diwani wa Kata
hiyo ya Utengule aliwahimiza wananchi wake kutokata tamaa na badala yake
waendelee kufanyakazi na kuunga kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali
katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Alisema kuwa,Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba,Mhandisi,Stephano Bulili Kaliwa amekuwa
mstari wa mbele katika kuzitafutia ufumbuzi kero na changamoto za wananchi
hususan wa kata ya Utengule.
Mhenga alisema kuwa toka alingie madarakani
mwaka 2020 amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mlimba,ambapo katika kata yake toka mwaka 2021 kwa nyakati tofauti kata yake
imepokea fedha za maendeleo zaidi ya milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule za msingi na sekondari,ujenzi wa zahanati na uchimbaji wa
visima.
Pia, alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kumteua Mhandisi
Stephano Bulili Kaliwa kuhudumu nafasi ya ukurugenzi kwa halmashauri ya Mlimba.
“Sisi wananchi wa Utengule
tunaimani kubwa kwa viongozi wetu wa halmashauri ya Mlimba pamoja na ofisi ya
mbunge wa Jimbo la Mlimba”alifafanua.
Alisema kuwa kata yake
wakati akipoingia madarakani alikuwa ikiwa na shule moja ya msingi lakini kwa
sasa kata yake ina shule ya msingi 5,alikuta maboma matatu lakini kwa sasa kata
hiyo ina miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa jengo la zahanati ya
kisasa.
No comments:
Post a Comment