Wadau wa Elimu watathmini Elimu ya sekondari kwa njia mbadala
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda ameridhishwa na hatua ya Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kufanya tathimini ya mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari na program ya sekondari kwa njia mbadala nchini (SEQIP-AEP) ikiwa ni hatua ya kuleta mageuzi ya elimu.
Prof.Mkenda amesema hayo mjini Morogoro wakati akifungua kikao cha tathmini ya mradi wa SEQIP-AEP uliogharimu dola za kimarekani mil.500 sawa na trilioni 1.2 iliyotolewa na benki ya dunia katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.
Alisema mradi huo unagusa maeneo mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu nchini umetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo matokeo yake yameonekana kutoka na ujenzi wa shule za sekondari mpya 830,ikiwemo shule za sayansi 26 kwa wasichana kwa kila mkoa hapa nchini.
Aidha,Prof.Mkenda alielezea juu ya uwepo wa mitaala mpya wa elimu ni sehemu ya mkakati wa kuboresha kwamba uendeshaji wa shule ya msingi utakuwa miaka 6,ambapo elimu ya lazima sasa itakuwa ni miaka 10 kwamba utekelezaji wake utafanyika kwa awamu.
Felista Mapunda ni Mratibu wa Elimu ya Watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Wizara ya Elimu,Sanyansi na Teknolojia akiongea kwa niaba ya Kamishna wa elimu nchini amesema kuwa ofisi ya Kamishna wa elimu ilikuwa ikitoa ushirikiano mkubwa katika kufikia malengo yaliokusudiwa na kupata matokeo chanja.
Mapunda anasema kuwa ofisi ya Kamishna wa Elimu imekuwa ikishirikiana na Taasisi ya watu wazima katika uandaaji wa miongozo mbalimbali yalioleta tija na mafanikio kwa kusajili wasichana 10,239.
Kwa upande wake,Mkuu wa Taasisi ya Watu wazima Prof. Michael Ng’umbi amesema kuwa kupitia mradi wa kuimarisha ubora wa elimu ya sekondari na programu ya elimu ya sekondari kwa njia mbadala nchini (SEQIP-AEP) umekuwa na tija ambapo amependekeza kuwa mradi huo uendelee kutekelezwa katika awamu ya pili.
Prof.N’gumbi alisema kuwa Taasisi ya watu wazima ni imekuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi wa SEQIP-AEP ulioanza kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2020/2021 hadi 2024/2025.
Mbali na hayo pia alisema kuwa taasisi hiyo mwezi Agosti mwaka huu wanatarajia kuadhimisha jubilee ya miaka 50 toka ilipoasisiwa ambapo kwa sasa wapo katika mchakato wa maandalizi ambapo kutakuwepo kwa shughuli za upandaji miti,madarasa ya ujasiriamali,Kongamano la kitaaluma,kuendesha elimu kwa umma juu ya uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.
No comments:
Post a Comment