MIAKA
4 YA DHAHABU YA RAIS SAMIA KUADHIMISHWA MOROGORO
Na Thadei Hafigwa
KONGAMANO kubwa la vijana
la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa
kutimiza miaka 4 toka aingie madarakani linatarajia kufanyika mjini Morogoro
Machi 19 mwaka huu na kuhudhuria wa mawaziri mbalimbali wa kisekta.
Mkuu wa idara ya uhusiano
wa kimataifa,vyuo vya kati na vyuo vikuu UVCCM,Emanuel Martine amebainisha hayo
mjini Morogoro wakati akiongea na waandishi wa habari kuelezea umuhimu wa
kongamano hilo ambalo Waziri wa Mipango Dkt.Kitila Mkumbo anatarajiwa kuongoza
timu ya mawaziri mbalimbali wa kisekta kuelezea jinsi mafanikio yaliopatikana katika
kipindi cha miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia kwa vijana.
Martine amesema kuwa Rais
Samia amefanya mambo mengi hivyo anapaswa kupewa maua yake hasa kwa kupanua
fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo upatikanaji wa ajira katika maeneo
mbalimbali hapa nchini,kwamba mawaziri hao wataainisha kwa kutoa takwimu sahihi
juu ya mafanikio hayo.
“ninapenda kuwaalika vijana wa mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani,kote nchini kushiriki kwenye kongamano hilo ambalo litatanguliwa na maandamano yatakayoanzia ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro vilizopo eneo la sabasaba hadi ukumbi wa tanzanite uliopo mjini Morogoro”alisema
Aidha,katika kongamano hilo
vijana watakapata fursa za kujadiliana mambo mbalimbali yaliofanywa na serikali
ya chama cha mapinduzi ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu
Hassan.
Sanjari na hilo,alisema
kuwa kongamano hilo litashirikisha
Mawaziri wa sekta mbalimbali,viongozi mbalimbali wa serikali,asasi za
kiraia ambao watapata fursa ya kuelezea mafanikio yaliopatikana katika kipindi
cha miaka 4 ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita hususan kwa upande wa
vijana.
Alitaja Kauli mbiu ya
Kongamano hilo ni “Wasomi Tumekuelewa Maendeleo Tumeyaona Dk Samia
Mgombea wetu” kwamba
katika kudhihirisha umuhimu wa kongamano hilo makundi mbalimbali yatashiriki
wakiwemo mama na baba lishe,bodaboda,wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga’ na
asasi.
Kwa
upande wake,Katibu wa umoja wa vijana CCM mkoa wa Morogoro,Vaileth Soka amewahimiza
vijana wanawake kushiriki katika kongamano hilo ambalo linatoa taswira ya umoja
na mshikamano katika jamii kwa kuwa mahitaji ya vijana yanafanana bila ya
kujali itikadi ya mtu.
Soka alisema ya kuwa katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuna mafanikio makubwa katika kada ya wanawake kwani zipo fursa nyingi zimeelekezwa kwa wanawake,hivyo muda wa kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wajitokeze na kuchagua viongozi wanaowataka katika kuimarisha demokrasia hapa nchini.


No comments:
Post a Comment