Breaking News

Mar 19, 2025

UVCCM WAJIVUNIA MAFANIKIO MIAKA 4 YA RAIS SAMIA MOROGORO

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa,Mohamed Kawaida akivishwa skafu muda mfupi baada ya kuwasili mjini Morogoro kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano la Miaka 4 ya Dhahabu ya Rais Samia Suluhu Hassan toka akingie madarakani.

UVCCM WAJIVUNIA MAFANIKIO MIAKA 4 YA RAIS SAMIA MOROGORO

Na Mwandishi wetu

KONGAMANO la kihistoria la mafanikio ya miaka 4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan toka angie madarakani limekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwakutanisha Mawaziri wawili wa kisekta mjini Morogoro Machi 19,mwaka huu wakibainisha mafanikio yaliopatikana ndani ya serikali ya awamu ya sita.

Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wamejitokeza kwa vingi kuungana na umoja wa vijana katika kongamano hilo ambalo limewashirikisha viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika ngazi tofauti ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan wakiwa na shauku ya kusimiliza taarifa za mafanikio zilizoandaliwa na Mawaziri wa Kisekta.

Mawaziri walioshiriki katika kongamano hilo la Dhahabu la Rais Samia ni pamoja na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Kitambi na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ambaye katika taarifa yake ya mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wa Rais Samia wa Miaka 4 katika sekta ya elimu alisema kuwa fedha za mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kutoka shilingi bilioni 464 mwaka 2021 hadi kufikia zaidi ya bil 700.

 Prof Mkenda amesema katika Kongamano hilo la dhahabu ya Uongozi wa Rais Samia lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda akiongea wakati wa Kongamano mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita,inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan Mjini Morogoro kwenye Kongamano.

"Kwa kipindi kifupi sana tangu mheshimiwa Rais aingie madarakani ameweza kuongeza mikopo ya elimu ya juu kutoka bilioni 464 na kufikia zaidi ya shilingi bilioni 700" alisema Waziri Mkenda

Aidha, Prof Mkenda akizungumzia ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za sekondari ambayo yamesaidia asilimia 75 ya  wahitimu wa darasa la saba ambao wanafaulu wanaanza kidato cha kwanza bila ya kikwazo chochote tofauti na hapo awali.

 Pia alisema kuwa  serikali imeteka zaidi ya trilioni moja kwa ajili ya kujenga kampasi za vyuo vikuu katika mikoa mbalimbali hapa nchini "Tumejenga shule nchi nzima kwa mfano wanaoenda kidato cha kwanza wanaenda kwa mkupuo wala hakuna kubaguana tena"amesema Waziri Mkenda

Patrobas Kitambi ni Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi,ajira na watu wenye ulemavu akitoa taarifa katika kongamano hilo juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia kwamba kuna mafanikio lukuki katika mabadiliko ya kisera katika sekta ya madini ambayo imesaidia kijana wa kitanzania kuwa katika kumiliki  kitalu cha madini tofauti na siku za nyuma.

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi,Ajira na Watu wenye ulamavu,Protabas Katambi akielezea mafanikio ya kijumla kisekta wakati akiongea katika kongamano la dhahabu ya miaka 4 ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan mjini Morogoro.

Kitambi alianisha kwa muhtsari wa kijumla katika maeneo mbalimbali baadhi yake ni ujenzi wa miundombinu ya treni ya kisasa ya SGR,kwamba treni hiyo imeshaanza kuwahudumia watanzania kwa kusafirisha abiria kutoka  mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro na Dodoma.

Aidha,alianisha maeneo ya miradi ya kimakakati inapotekelezwa vijana wanapata ajira ya moja kwa moja na nyingine za muda mfupi,pia jamii inayopitiwa na miradi ya aina hiyo wananufaika kwa kufanya biashara ndogondogo katika huduma ya mama lishe na kujiongezea kipato.

Mgeni wa Kongamano hilo ni Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Taifa Mohamed Ali Kawaida katika hotuba yake amewaasa vijana kuhakikisha ya kuwa CCM katika uchaguzi mkuu wa Urais,Ubunge na Madiwani inashinda.

                        Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa(UVCCM),Mohamed Kawaida

Kawaida alisema kuwa vijana wa ccm wanawajibu wa kulinda amani ya Tanzania,na kwamba wasinyumbishwe na mtu wala wanasiasa wasiyoitakia mema nchi kwa kutoa matamshi yenye niashiria vya kuleta vurugu ndani ya nchi.

Pia, alitoa rai kwa vijana wa vyuo vikuu hapa  nchini kuepuka vyama vinavyohubiri uvunjifu wa amani  pamoja na kuwagawa Watanzania kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira.

"Nikuombeni sana ndugu zangu wasomi,acheni kusikiliza maneno ya fitina na porojo,kwa sababu sisi ni wasomi tutumie elimu yetu kutafakari na kuchuja mambo"amesema

Awali kongamano hilo lilitanguliwa na shamrashamra za maandamano ya bodaboda,vijana kutoka wilaya mbalimbali mkoani Morogoro na kuwashirikisha viongozi wa umoja wa vijana wa CCM kutoka Mikoa ya Kilimanjaro,Tabora,Singida na Shinyanga.

Mbali na hao,Kongamano hilo lilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Musa Kilakala ambaye alielezea mafaniko yaliopatikana katika uongozi wa Rais Samia ni pamoja na ujenzi wa bwawa la Kidunda ambalo mpaka kukamilika kwake litagharimu shilingi bil.336 .

Kilakala alisema mradi huo wa maji utapunguza kero ya maji kutoka mikoa ya Morogoro,Pwani na Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment