Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda
MAWAZIRI WA KISEKTA WAELEZEA MAFANIKIO MIAKA 4 YA RAIS SAMIA
Na Thadei Hafigwa
KONGAMANO kubwa la kihistoria la
mafanikio ya miaka 4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia
Suluhu Hassan toka angie madarakani limekuwa na mafanikio makubwa kwa
kuwakutanisha Mawaziri wawili wa kisekta mjini Morogoro Machi 19,mwaka huu wakibainisha
mafanikio yaliopatikana ndani ya serikali ya awamu ya sita ikiwemo elimu,miundombinu na madini.
Mawaziri walioshiriki katika kongamano hilo la Dhahabu la Rais Samia ni pamoja na Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,Ajira na Watu wenye ulemavu,Patrobas Kitambi na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia katika taarifa yake ya
mafanikio yaliyopatikana katika uongozi wa Rais Samia wa Miaka 4 katika sekta
ya elimu alisema kuwa fedha za mikopo ya elimu ya juu imeongezeka kutoka
shilingi bilioni 464 mwaka 2021 hadi kufikia zaidi ya bil 700.
Prof Mkenda amesema katika Kongamano hilo la
dhahabu ya Uongozi wa Rais Samia lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi(UVCCM) Taifa kwamba,
"Kwa kipindi kifupi
sana tangu mheshimiwa Rais aingie madarakani ameweza kuongeza mikopo ya elimu
ya juu kutoka bilioni 464 na kufikia zaidi ya shilingi bilioni
700",alisema Waziri Mkenda
Aidha, Prof Mkenda akizungumzia
ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za sekondari ambayo yamesaidia
asilimia 75 ya wahitimu wa darasa la
saba ambao wanafaulu wanaanza kidato cha kwanza bila ya kikwazo chochote
tofauti na hapo awali.
Pia alisema kuwa serikali imeteka zaidi ya trilioni moja kwa
ajili ya kujenga kampasi za vyuo vikuu katika mikoa mbalimbali hapa nchini "Tumejenga shule nchi nzima kwa mfano wanaoenda kidato cha
kwanza wanaenda kwa mkupuo wala hakuna kubaguana tena"amesema Waziri
Mkenda
Patrobas Kitambi ni Naibu
Waziri ofisi ya Waziri Mkuu kazi,ajira na watu wenye ulemavu akitoa taarifa
katika kongamano hilo juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha
uongozi wa Rais Samia kwamba kuna mafanikio lukuki katika mabadiliko ya kisera
katika sekta ya madini ambayo imesaidia kijana wa kitanzania kuwa katika kumiliki kitalu cha madini tofauti na siku za nyuma.
Kitambi alianisha kwa
muhtsari wa kijumla katika maeneo mbalimbali baadhi yake ni ujenzi wa
miundombinu ya treni ya kisasa ya SGR,kwamba treni hiyo imeshaanza kuwahudumia
watanzania kwa kusafirisha abiria kutoka
mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro na Dodoma.
Aidha,alianisha maeneo ya
miradi ya kimakakati inapotekelezwa vijana wanapata ajira ya moja kwa moja na
nyingine za muda mfupi,pia jamii inayopitiwa na miradi ya aina hiyo wananufaika
kwa kufanya biashara ndogondogo katika huduma ya mama lishe na kujiongezea
kipato.
Mgeni wa Kongamano hilo ni
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Taifa Mohamed Ali
Kawaida katika hotuba yake amewaasa vijana kuhakikisha ya kuwa CCM katika
uchaguzi mkuu wa Urais,Ubunge na Madiwani inashinda.
Kawaida alisema kuwa vijana
wa ccm wanawajibu wa kulinda amani ya Tanzania,na kwamba wasinyumbishwe na mtu
wala wanasiasa wasiyoitakia mema nchi kwa kutoa matamshi yenye niashiria vya
kuleta vurugu ndani ya nchi.
Pia, alitoa rai kwa vijana
wa vyuo vikuu hapa nchini kuepuka vyama
vinavyohubiri uvunjifu wa amani pamoja
na kuwagawa Watanzania kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira.
Nikuombeni sana ndugu zangu
wasomi,acheni kusikiliza maneno ya fitina na porojo,kwa sababu sisi ni wasomi
tutumie elimu yetu kutafakari na kuchuja mambo"amesema
Awali kongamano hilo
lilitanguliwa na shamrashamra za maandamano ya bodaboda,vijana kutoka wilaya
mbalimbali mkoani Morogoro na kuwashirikisha viongozi wa umoja wa vijana wa CCM
kutoka Mikoa ya Kilimanjaro,Tabora,Singida na Shinyanga.
Mbali na hao,Kongamano hilo
lilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Musa Kilakala ambaye alielezea
mafaniko yaliopatikana katika uongozi wa Rais Samia ni pamoja na ujenzi wa
bwawa la Kidunda ambalo mpaka kukamilika kwake litagharimu shilingi bil.336 .
Kilakala alisema mradi huo
wa maji utapunguza kero ya maji kutoka mikoa ya Morogoro,Pwani na Dar es
Salaam.

No comments:
Post a Comment