Doyo Hassan Doyo(Pichani) Akisisitiza jambo wakati alipoongea na waandishi wa habari mjini Morogoro kuhusu dhamira yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha NLD.
DOYO WA NLD ALETA FUKUTO LA KINYANG’ANYIRO CHA URAIS NDANI YA CHAMA CHAKE
Na Thadei Hafigwa
WAKATI vyama vingine vya siasa vikijiweka mguu sawa kuelekea uchaguzi mkuu wa Urais,Ubunge na Udiwani hapa nchini unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu mwanachama wa Chama cha Nation League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo amekutana na waandishi wa habari na tangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Doyo amebainisha vipaumbe 10 ambavyo kwa mtazamo wake iwapo akipitishwa na chama chake ndivyo akavyovinadi kwa watanzania kwenye majukwaa ya siasa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa
habari mjini Morogoro Machi 14.2025, Doyo ametaja vipaumbele hivyo ni ajira,
elimu, kilimo na ufugaji, rasilimali za maji, kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi.
Kipaumbele vingine ni
pamoja na kupambana na rushwa kwa
kiwango kikubwa na kujenga taifa la walipa kodi kwa kiwango kinachostahili,hata
hivyo amechukua fursa hiyo kuipongeza mamlaka ya mapato nchini kwa jitihada
zake za kukusanya mapato.
Aidha,Doyo kwa mtazamo wake
haoni sababu ya chama chake kuungana na vyama vingine kuing’oa CCM madarakani
kwa kuwa chama hicho kimesheni wanachama wenye sifa na uweledi wa kushika dola.
Amesema kuwa chama chake
kitasimamisha wagombea ubunge nchini nzima na pia baadhi ya maeneo watasimamia
wagombea katika nafasi ya udiwani kwa kuwa wamejipanga vema katika kuhakikisha
wapiga kura wao wamejiandikisha katika daftari la kudumu la kupika kura.
“iwapo nikipitishwa na
chama change kuwa mgombea,kipaumbe change kikubwa ni kupambana na suala ajira
ambayo limekuwa ni tatizo kubwa tunao wasomi wamemaliza vyuo vikuu lakini
hawajapata ajira rasmi baadhi yao wanajihusisha na sekta ya usafirishajiwa
abiria kwa bodaboda”alisema na kuongeza kuwa
“siibezi ajira ya bodaboda
bali mazingira waliokuwa nayo wasomi wetu waliohitimu vyuo vikuu kwa
kujihusisha na shughuli za bodaboda inapunguza hadhi ya elimu yetu hapa nchini.”
Mbali na hayo amejinasibu
kwa kuweka vipaumbele vingine ni pamoja na kuweka nguvu katika sekta ya madini,
kuongeza jitihada kwa watoto wa kike katika kupata elimu ya teknolojia.
Kadhalika kwa mtazamo wake
amesema atahakikisha wanaimarisha Muungano wa Tanzania na kuimarisha sekta ya
binafsi katika kukuza na kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
ikiwemo sekta ya madini.
Pia,hakusita kutaja baadhi
ya mafanikio yaliyopatikana katika serikali ya awamu ya sita ikiwemo SGR,bwawa
la kufua umeme la Mwalimu Julius Nyerere,ujenzi wa vyuo vikuu nchi ambapo
wakati taifa lililopata uhuru kulikuwa na chuo kikuu kimoja.
Katika mkutano huo, Doyo
aliongozana meneja wake, Twaha Saidi Mngatwa na familia yake, mkuu wa itifaki,
Kibi Saidi Amri.Kwa upande wake Twaha Saidi Mngatwa meneja wa mtia nia (mgombea),
amebainisha kuwa baada ya kutangaza nia ya bosi
wake kugombea nafasi ya urais atachukua fomu katika chama chake Machi 21 na ifikapo
April 10 kutafanyika uteuzi ndani ya chama atapeperusha bendera ya kunadi sera
za chama katika mikutano ya kampeni baada ya kupitishwa na tume huru taifa ya uchaguzi.

No comments:
Post a Comment