Breaking News

Nov 5, 2024

Chama Cha MDAG Wapongeza Jeshi la Polisi


Seleman Idd,Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Madereva(MDAG)

Na Mwandishi wetu

Chama Cha Madereva Cha Mkombozi Driving African Group (MDAG) wamelipongeza Jeshi la Polisi Chini kwa kazi nzuri ya usimamizi wa Sheria ya usalama barabarani ambapo imesaidia kupunguza ajali barabarani,hapa nchini.

seleman Iddi ni rais wa umoja wa madereva hao(MDAG) ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ambapo blog hii ni miongoni mwa waliofanikiwa kupata taarifa hii, kwamba madereva licha ya kukabiliwa na  changamoto nyingi katika utendaji wao wa kazi kutokana na kufanyakazi zinazohatarisha maisha yao lakini wana Imani kubwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika kuweka mazingira rafiki katika uendeshaji wa Nchini kutokana na falsafa yake ya 4R.

Idd amesema kuwa madereva wengi wa malori hawana mikataba ya kazi,bima kwamba hata malipo wanayopewa ni madogo hayakidhi mahitaji ya kuwasaidia wao na familia zao.

"Sisi tunalipwa mishahara na waajiri wetu kati ya 300,000 hadi 500,000 ,posho ya safari ni kati 700,000 Hadi 800,000 hii haitoshi ukiringanisha na kazi tunazifanya,tunasafiri nje ya nchi,congo na nchi nyingine huko wanatumia Dola,sisi mabosi wetu wanatupa fedha za hapa nyumbani,hii ni changamoto kubwa kwetu" alisema

Alisema kuwa kupitia chama chao wanapendekeza kuwa malipo kwa madereva wa maroli wanaosafiri nje ya nchi walipwe mshahara wa Dola 500 sawa na shilingi mil 1.3 kwa fedha za kitanzania,sanjali na kupatiwa posho katika mfumo wa malipo kwa dola 200 Hadi Dola 300 ya safari ili kuwarahisishia gharama za maisha wanapokuwa nje ya nchi 

Aidha,alisema kuwa chama chao Cha  MDAG nimependekeza mshahara na posho zao zilipwe na waajiri wao(mabosi),kwamba Wana Imani kubwa na serikali kwamba changamoto wanazopata  zinapatiwa ufumbuzi.

Alisema kuwa serikali ikifuatilia na kusimamia mifumo hii ya mikataba kwa madereva wa maroli itakuwa imemaliza tatizo hilo la ambalo amedai ni la muda mrefu.

Sambamba na hayo,alisema kuwa jamii inapaswa kuuelewa na kutambua mchango wa madereva katika sekta ya usafirishaji katika ulinzi na usalama kwenye sekta ya miundombinu,kwamba wapo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na mamlaka zake zote.

No comments:

Post a Comment