MADEREVA WATAKA MIKATABA YA AJIRA KUPITIA CHAMA CHA MADEREVA MDAG
Na Mwandishi wetu
ILI kukabiliana na matukio ya vitendo vya uharifu,wizi chama cha madereva wametaka wamiliki wa vyombo vya usafiri kushirikiana na chama cha madereva nchini katika uandaaji wa mikataba ya madereva ili kuepuka usumbufu wanaopata wamiliki kwa matukio ya wizi.
Wito huo umetolewa na rais wa Chama cha madereva cha Mkombozi,Seleman Idd (MDAG) katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa matukio ya madereva kuwekwa mahabusu kwa madai ya wizi wa mafuta na mizigo yanasababishwa na uwepo wa mazingira yasiyo rafiki yaliopo mikataba ya ajira zao.
Idd alisema kuwa muarobaini wa matukio ya wizi ni chama chake cha MDAG kukaa meza moja na umoja wa wamiliki wa magari (TATOA) ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo kabla ya dereva hajaanza kazi inapaswa mikataba hiyo ikipitie kwa chama cha madereva ili kulinda masilahi ya pande zote mbili.
alisema kuwa wamiliki wa magari wanapotaka madereva walipitie kwenye chama,hali hiyo itasaidia kupunguza malalamiko yaliopo kutoka kwa wamiliki wa magari kuibiwa mafuta na mizigo inayosafirishwa.
Hata hivyo alisema mbali ya kuwepo chama cha madereva lakini Chama cha TATOA ambacho nikihusisha wamiliki wa magari ndiyo wenye maamuzi ya mwisho. “madereva wengi wanatambua kwa nini matukio ya wizi yanatokea,ni wapi wanapotokea wizi.chanzo kikuu ni madereva kukosa stahiki zao kwa wakati.”alisema
Alisema kuwa madereva wanafanyakazi katika mazingira magumu,kwamba malipo wanayopata yamegumikwa na utata kwa kuwa wanasafiri bila kupewa staiki zao kwa wakati,wanatoka Dar es Salaam bila ya kuwa na malipo wanalazimika kuegesha gari wakiwa njia,Morogoro,Dumila wakisubiri kuingiziwa fedha za safari kwenye simu hali hiyo imekuwa ni kero kubwa.
Alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili madereva ni pamoja na kuwekwa mahabusu ndani na nje ya nchi kwa makosa mbalimbali, kutokuwa na bima ya afya,mfuko wa jamii,bima ya kifo na bima ya ajali. kwamba iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa madereva wataendelea kuteseka pamoja na familia zao.
“Madereva wengi wapo mitaani wamevunjika miguu,wengine wamepoteza maisha kutokana na kukosa bima ya ajali,kifo kwamba wanateseka sana wamekuwa omba omba.”alisema.
Alisema kuwa wadereva wanategemea malipo yao ili kuwahudumia watoto wao,kwa kuwalipia ada,matibabu pamoja na mahitaji mengine ya msingi lakini kwa sababu ya hali ilivyo sasa kuna haja ya vyama viwili kukaa meza moja TATOA na MDAG ili kuboresha masilahi ya madereva ambao kazi yao ni ya hatari.
No comments:
Post a Comment