Breaking News

Oct 26, 2024

KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA YAWASOGEZEA HUDUMA WATEJEA SGR MOROGORO

Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba(katikati) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Paschal Kihanga aliyevaa shuti kushoto,mara baada ya uzinduzi wa Duka la Airtel lililozinduliwa ofisi ya SGR kituo cha Morogoro(Picha na Thadei Hafigwa)

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

IMEELEZWA kuwa uwepo wa treni ya kisiasa ya SGR imeongeza kasi ya uwekezaji katika miundombinu ya mawasiliano baada ya kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kujitokeza kuunga mkono serikali kwa kuweka huduma zao kwenye zao kwenye kituo cha Morogoro.

 Sambamba na hiyo, halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inakusudia kuanza ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa ili kuwapunguzia mzigo wa gharama wasafiri wanatumia usafiri wa Treni ya Mwendokasi (SGR) takribani kasi yake kuongeka.

Meya wa Manispaa wa Morogoro,Pascal Kianga alisema ujenzi wake utaanza wakati wote kuanzia sasa baada kupatikana kwa Mkandalasi na kwamba ametaka wakazi wa Manispaa hiyo kutumia fursa ya kuwepo  kwa Treni ya SGR kwa kubuni biashara mbalimbali zitakazo waingizia kipato.

Meya Kianga alisema hayo wakati akizindua Duka la Kisasa la Kampuni ya mawasiliano ya Simu ya Airtel Tanzania  lilojengwa kwenye stendi hiyo ya SGR kwa ajili ya kurahisha wasafiri wanaingia na kutoka nje ya mkoa wa Morogoro.

Mwigizaji wa filamu na michezo ya runinga kutoka nchini Tanzania,(Joti) watatu kutoka kushoto ambaye pia ni balozi wa artel Tanzania,akishuhudia zawadi iliyotolewa na kampuni hiyo kwa Diwani wa Kata ya Kimamba 'B',Willie Mathew wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel katika kituo cha Treni ya Kisasa SGR kituo cha Morogoro,wengine walishuhudia zoezi hilo ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Pascha Kianga,na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Tanzania,Adriana Lyamba.(Picha na Thadei Hafigwa)

Inakadiriwa kuwa wasafiri zaidi ya 1000 wanatumia treni hiyo ya kisasa kwa siku huku wakiwa na mahitaji mbalimbali ya huduma ya mawasiliano.

Alisema fursa nyingine ni pamoja na Manispaa hiyo kuanza kujipanga kuwa Jiji tarajiwa kwakuanza kuboresha miundo mbinu ya mawasilino yatakayorahisha wananchi kupata huduma za kijamiii.

“Niwaombe  wananchi kuchangamkia fursa iliyopo ya SGR inayofanya safari zake Morgoro Dar es Salaam na Dodoma kwa siku kuna abiria zaidi ya 10000 wanaingia na kutoka wanakuja kuanzia safari hao kwenda mikoa mbalimbali watumiea nafasi hiyo kujipanga kufanya shughuli za ujasilimali wasisubiri waje kutoka nje ya mkoa wakati wao wapo hapahapa” alisema Meya Kianga

Alisema Manispaa imeboresha miundombinu ya mawasiliano ambayo kati ya Kata 29 mpaka sasa ni kata moja tu yenye changamoto hiyo ambayo siku chache zijazo tatizo hilo litamalizika.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania,Adriana Lyamba,alisema wameamua kuwasogezea huduma wasafiri wanaotumia Treni hiyo ya Mwendokasi kwenye stendi hiyo ili kupata huduma zote wakiwa kwenye maeneo bila kwenda mjini.

Alisema Airtel imekuwa ikiunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali ikiwemo kusogeza huduma kwa wananchi ili kuwapunguzia adha ya kutumia umbali mrefu kuzifuata huduma hizo.

Katika hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Lucas Lazaro Mhuvile (Joti),mwigizaji wa filamu na michezo ya runinga kutoka nchini Tanzania ambaye ni Balozi wa kampuni ya Airtel Tanzania.

Joti ambaye akiwa balozi wa kampuni ya Airtel Tanzania,amewahimiza watanzania kuhakikisha wanatumia huduma kedekede zinazotolewa na Kampuni hiyo kutokana na jinsi inavyojipambanua katika utoaji wa huduma kwa kuwa karibu na wateja

No comments:

Post a Comment