Na Thadei Hafigwa,Morogoro
KATIKA kukabiliana na changamoto za matukio utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wasio na uadilifu jamii imeaswa kuhifadhi fedha katika taasisi za fedha.
Meneja wa benki ya NMB, tawi la Wami, Victor Mboya ,amebainisha hayo katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa baadhi ya wateja wao wanaotumia taasisi hiyo katika uhifadhi wa fedha.
Mboya amesema taasisi hiyo ina wajibu wa kutoa elimu ya kutunza fedha kwa wasio wateja wao.Kwamba watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea kidogo kidogo kwa matumizi ya baadae.
Meneja wa huduma kwa wateja Benki ya NMB tawi Wami,Victor Mboya akimkabidhi Amosi Mayila (aliyevaa t shirt ya rangi ya machungwa)zawadi ya TV inchi 75 baada ya kuibuka mshindi katika droo ya 4.Amesema kuwa benki ya NMB baada ya kuona umuhimu wa kuweka akiba katika taasisi yao,wameamua kuweka zawadi ili kuhamasisha wateja kuendelea kuweka akiba kupitia kampeni ya bonge la mpango mchongo ndio huu.
Amosi Mayila (22) mkazi wa Ruaha Mkoani Morogoro pamoja na George Ambukege (32) ni baadhi ya wateja waliokabidhiwa Tv inchi 75 friji kutoka benki ya NMB baada kuibuka mshindi katika droo ya nne.
Aidha,kwa upande wake Amos Mayila ambaye alipokea zawadi ya TV inchi 75 amesema ataitumia zawadi hiyo kama moja ya chanzo cha kujiongezea kipato katika familia yake.
Washindi wengine Shila Gabriel(Manyoni),Joseph Mollel(Singida) na Regins chiwa ambalo kila mmoja katika droo hiyo walijipatia kitita cha shilingi laki moja.
Katika kampeni hiyo mshindi wa jumla atajishindia kitita cha shilingi milioni mia moja na zawadi nyingine mbalimbali ikiwemo friji,mashine ya kufulia na jiko la gesi.
Kampeni hiyo imeanza septemba 25 ambayo itakuwa ni kipindi cha miezi mitatu na inatarajia kuhitimika Desemba 19 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment