HYDROXYCHLOROQUINE BADO HAIJATHIBITISHWA KUWA INAPONYA AU KUTIBU COVID-19
Na Juma Mtanda
Dawa za
Hydroxychloroquine na chloroquine hutumika kwa matibabu ya malaria na magonjwa
mengine licha ya kuwepo kwa uvumi kuwa dawa hiyo zinaweza kuponya covid 19
Kwa mujibu wa shirika
la afya duniani inaeleza kuwa, utafiti uliofanywa kuwa dawa hizo
zina viashiria ya kuweza dawa hizo
zinazoweza kuwa tiba kwa COVID-19, lakini data iliyopo kwa sasa inaonyesha
kwamba hazipunguzi vifo kutokana na COVID-19 au kusaidia watu walio na ugonjwa
wa wastani.
Tanzania licha ya kuwa
ni sehemu ya dunia ambayo inakabiliwa na covid 19 lakini wananchi wake wapo
salama na wanaendelea kuchapa kazi,hii inatokana na serikali ya awamu ya tano
kuwahamasisha wananchi kumrejea Mungu ili awanusuru watanzania dhidi ya ugonjwa
huo.
Wananchi wa Mjini Morogoro na vitongoji vyake wamekuwa wakichukua tahadhali na umakini wa kipekee kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wanakuwa salama wakati wote licha ya kuwepo wa mwingiliano katika shughuli za kiuchumi.
taarifa hiyo ya WHO,inaeleza kuwa dawa ya Hydroxychloroquine na chloroquine zinaweza kutibu malaria na magonjwa ya kinga otokamtiki ya mwili. Hata hivyo, kuzitumia kutibu magonjwa mengine, bila uangalizi wa kimatibabu kunaweza kusababisha madhara mabaya zaidi na kunapaswa kuepukwa.

No comments:
Post a Comment