UN PHOTO/ESKINDER DEBEBE
KATIBU MKUU WA UN ANTÓNIO GUTERRES
AKIPATIWA CHANJO YA COVID-19 KWENYE SHULE MJINI BRONX NEW YORK
KATIBU WA UMOJA WA MATAIFA NA NDOTO YA KUTOKOMEZA COVID 19
Ripota wetu,
MOROPC BLOG KWA MSAADA WA HABARI UN
KATIKA kuhakikisha ya kuwa duniani
inaendelea kuwa salama dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo covid 19,Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema chanjo dhidi ya corona au
COVID-19 ni muhimu ili kuhakikisha kila mtu kila mahali yuko salama dhidi ya
janga hili hatari.
Guterres amesema hayo muda mfupi baada ya
kuchomwa chanjo dhidi ya COVID-19 kwenye eneo la Brox jijini New York
Marekani katika zoezi linaloendelea la kuwapa chanjo kwanza makundi ya watu
walio hatarini zaidi kupata ugonjwa huo wakiwemo walio na umri wa zaidi ya
miaka 65.
Kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa
wake wa twitter mara baada ya chanjo hiyo Guterres amesema
“Nimebahatika na ninashukuru kupata dozi ya kwanza
ya chanjo yangu ya COVID-19 leo. Ni lazima tufanyekazi pamoja kuhakikisha
kwamba chanjo inapatikana kwa kila mytu kila mahali. Kwa janga hili hakuna
aliyesalama haki pale kila mtu atakapokuwa salama.”
Kwa hatua nyingine, wakazi wa Manispaa ya Morogoro wamehamasika kufuata kanuni za afya zilizotolewa na wadau mbalimbali wa afya kwa kunasa maji tiririka ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo covid 19.

No comments:
Post a Comment