DIWANI WA KATA YA TANGINI,KIBAHA-PWANI,MFALME KABUKA KUSHOTO KATIKATI ALIYENYANYUA MKONO WAKE KUSISITIZA JAMBO KWA WAFANYABIASHA WADOGOWADOGO (HAWAPO PICHNI)
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Diwani wa Kata ya Tangini iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha
mji kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Mfalme Kabuka amewaasa
wafanyabiashara kuhakikisha kwamba wanazingatia usafi katika maeneo yao ya biashara.
Akizungumza na baadhi ya wafanyabishara wadogo wadogo wanaofanya
shughuli zao katika soko la Mnalani kuhusiana na mikakati yake
aliyojiwekea baada ya kuchaguliwa katika kuimarisha hali ya
usafi wa mazingira kwa lengo la kuweza kuwa na afya njema kwa wananchi na
kuondokana na magonjwa mbali mbali ya mlipuko.
“Mimi Kama Diwani wa Kata hii ya Tangini lengo langu kubwa ni
kuweka mipango ambayo itaweza kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika
soko hili la mnalani ,hivyo nitashirikiana bega kwa bega na viongozi wenzangu
wa halmashauri ili kuweza kuwapa fursa wafanyabiashara kufanya kazi zao bila ya
kupata magonjwa yoyote ya mlipuko kama vile kipindupindu, na magonjwa mengine
ambayo yanasababisha na uchafu wa mazingira.
Aidha alibainishwa kwamba katika kuunga juhudi za agizo la
Makamu wa Rais Mama Sami Suluhu la kufanya usafi wa mazingira katika kila
jumamosi ya mwisho wa mwezi amedai kwa upande wake atawashirikisha wananchi
wake ili kuhakikisha kwamba wananeo yote yanakuwa katika hali ya usafi kwa kufanya
usafi huo kwa kila mwisho wa juma la wiki.
“Katika Soko letu la Mnarani bado kuna baadhi ya changamoto
ambazo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kama vile kuweka mikakati ya
miundombinu mizuri ya maji ili mvua inapoanza kunyesha maji yasiweze kukwama na
pia kuweka sehemu maalumu kwa ajili ya shimo la kutupiatakakata hii itaweza
kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na magonjwa ya mlipuko,”alisema Kabuga.
Katika hatua nyingine, Diwani huyo, alitoa wito kwa wafanyabiashara
wote kuachana na tabia ya kutupa, takataka ovyo, na badala yake wahakikishe
wanaweka utaratibu za kuziweka sehemu moja ili ziweze kuchukuliwa kwa utaratibu
uliopangwa na kwenda kuzichoma katika sehemu ambayo imepangwa maalumu.
Pia aliongeza kuwa katika kukabiliana na wimbi la magonjwa mbali
mbali ya mlipuko wananchi wote wanapashwa kuendesha shugghuli zao kwa
kuzingatia sheria za na taratibu ambazo zimewekwa na kuheshimi miongozo yote
ambayo inatlewa na wataalamu wa afya lengo ikiwa ni kuweza mazingira yawe
katika hali ya usafi.
Pia Diwani huyo alimpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe
Magufuli kwa juhudi zake ka kuboresha sekta ya afya pamoja na kupambana vilivyo
na kufanikiwa kumalizika kabisa kwa ugonjwa wa Covid 19 ambapo aliweza kufanya
juhudi za makusudi hadi kufikia hatua ya kuumaliza kabisa katika maeneo mbalimbali.

No comments:
Post a Comment