MGANGA MKUU WA MKOA WA PWANI ,GUNINI KAMBA
MGANGA
MKUU PWANI AKEMEA WANAFUNZI KUJISAIDIA OVYO
NA
VICTOR MASANGU, PWANI
MGANGA Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Gunini Kamba amewawatahadharisha na kuwaonya vikali,
baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari kuachana kabisa
na vitendo vya kujisaidia katika maeneo ya vichaka kwani kufanya hivyo
kunaweza kusababisha madhara makubwa ya kutokea kwa mlipuko wa magonjwa
mbalimbali ikiwemo kipindupindu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake,kuhusiana
na mikakati waliyojiwekea katika ngazi ya Mkoa katika kupambana na
kudhibiti hali ya kuwepo kwa magonjwa ya mlupiko katika maeneo mbalimbali
hususan, katika mkusanyiko mkubwa wa watu kama vile mashuleni.
“Kwa sasa hivi tupo katika msimu mpya wa mwaka wa 2021 ambapo
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tayari wamefungua shule zao na kuanza
masomo lakini pamoja na mambo mengine yote ni lazima sisi kama wataalamu wa
afya tuweke mipango madhubuti ya kuwalinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki
na kuwatahadharisha na kutojisaidia ovyo katika maeneo ya vichaakni kwani hii
ni hatari sana kupata magonjwa ya mlipuko” alisema.
Aidha, Kamba alifafanya kubwa kwa kipindi hiki cha ni lazima
viongozi wa shule pamoja na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kwamba
wanazingatia maagizo ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia
usafi wa mazingira pamoja na kuweka mafi safi na salama katika maeneo ya shule
ili wanafunzi wanapotoka kujisaidia waweze kusafisha na kunawa mikono yao kwa
lengo la kuthibiti milipuko ya magonjwa hayo.
Pia, aliongeza kuwa katika kupambana na wimbi la mlipuko wa
magonjwa wanaendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu wa shule mbali mbali
zilizopo katika Mkoa wa Pwani juu ya kuwaelimisha umuhimu wa usafi wa
mazingira katika maeneo yao ya kazi na kuwapa mafunzo ambayo yataweza
kuwasaidia katika kuwaelimisha watoto wao katika kujikinga na magonjwa ambayo
yanatokana na uchafu.
“Suala la baadhi ya wanafunzi au jamii yoyote kuwa na tabia ya
kujisaidia katika maeneo ya vichakani hii sio sahii kabisa hata kidogo kwani ni
hatari zaidi kutokea kwa magonjwa ya milipuko kama vile kuumwa na tumbo,kuhara
na kuibuka kwa ugonwa wa kipindipindu na kitu kingine mtu anaweza
kujisaidia na mvuaikaja kunyesha hivyo ikikisomba kinyesi kunaweza kuleta
madhra makubwa katika jamii ambayo ipo karibu na maeneo hayo.
Katika hatua nyingine Kamba aliongeza kuwa serikali ya awamu ya
tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya na
kuwapatia huduma ya matibabu wananchi wake hivyo isingependa kuona hali ya
kuwepo kwa magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kuthibitiwa endapo jamii
ikizingatia kanuni na taratibu zote ambazo zinatolewa na watalaamu wa
sekta ya afya ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

No comments:
Post a Comment