NAIBU MKUU WA TAKUKURU MKOA WA PWANI,
SADIKI NOMBO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI)TAKUKURU PWANI YAOKOA ZAIDI YA MIL.58 KATIKA OPERESHENI ZAKE
VICTOR MASANGU, PWANI
TAASISI ya
kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuoko zaidi
ya shilingi milioni 58, ambazo zimetokana na malalamiko yaliyowasilishwa
yakiwemo ya wimbi la ubadhilifu wa fedha ambazo wamedhulumiwa
wakulima wa zao la korosho ikiwemo vikundi vya vijana
wanawake na walemavu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, Naibu
mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani, Sadiki Nombo,katika utekelezaji wa
majukumu yao katika kipindi cha miezi mitatu(robo mwaka) kuanzia mwezi Octoba
hadi kufikia Disemba mwaka 2020 pamoja na mikakati waliyojiweke katika kukabiliana
na wimbi la rushwa.
Aidha, alifafanua kuwa katika robo ya kuanzia mwezi octoba
hadi disemba mwaka 2020 Ofisi ya Takukuru iliweza kupokea mamalamiko yapatayo
196, ambapo kati ya hayo malalamiko 113 uchunguzi wake bado endelea
kufanyika ili kuweza kuwabaini wale wote waliohusika na sheria iweze kufuata
mkondo wake.
Pia, alielekeza kuwa katika utekelezaji huo, Takukuru Wilaya ya
Mkuranga waliweza kuokoa kiasi cha shilingi milioni 18 ambazo zilizotoka na
baadhi ya wakulima kudhulumiwa na viongozi wa bodi ya Amcos ya kimanzichana
kusini.
Kadhalika, katika Wilaya ya Kibiti Takukuru iliweza kuokoa kiasi
cha shilingi zaidi ya shilingi milioni 18 ambazo ziliweza kuokolewa kutoka
katika vikundi mbalimbali ikiwemo kwa vijana, wanawake pamoja na walemavu
ambavyo vilikopeshwa na halmashauri hiyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Alifafanua kuwa, kupitia katika Ofisi ya Wilaya ya Kisarawe
waliweza kufanya uchunguzi wa kina na kuweza kuokoa zaidi ya shilingi
milioni nne ambazo ziliweza kuchangwa na wananchi wa kijiji cha Marui Ngwata,kwa
ajili ya kufanya ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji hicho.
Kwa upande wa Ofisi ya Chalinze, katika kipindi cha mwezi octoba
hadi disemba mwaka 2020 iliweza kufanikia kurejesha kiasi cha shilingi milioni
moja zikiwa ni sehemu ya shilingi milioni tano ambazo zimetokana na mikopo ambayo
ilitolea kwa vikundi vya wanawake vijana pamoja na watu wenye ulemavu.
Ofisi ya Takukuru, Wilaya ya Kibaha, waliweza kufanya uchunguzi
na kuweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa wanunuzi wa dawa za
kituo cha afya cha Mlandizi ambapo manunuzi hayo yalikiukwa na utaratibu
haukuzingatiwa ipaswavyo kwani dawa ziliozagizwa kutoka kampuni binafsi ya
Astra Pharma Limited.
Katika hatua nyingine, Naibu huyo alibainisha kwamba, Takukuru
katika kupambana na wimbi la rushwa ya ngono ambayo imeonekana kuwa
ni changamoto kubwa katika baadhi ya maeneo hususan kwa wanafunzi
wameanzisha kampeni maalumu ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi
kupunguza hali hiyo.
Takukuru Mkoa wa Pwani katika robo ya tatu kuanzia mwezi octoba hadi disemba mwaka 2020 imeweza kupokea kesi zipatazo 27 ambazo zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali pamoja na kupokea malalamiko yapatayo 196 ambapo kati ya hayo malalamiko 113 yapo katika hatua ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment